Ukurasa huu unaleta pamoja taarifa kuhusu muongozo kutoka kwa Shirika la afya la Umoja wa Mataifa, WHO na Umoja wa Mataifa kuhusu mlipuko wa sasa wa virusi vya corona au COVID-19, ambavyo viliripotiwa mara ya kwanza Wuhan, China mnamo Desemba 31, 2019. Tafadhali tembelea ukurasa huu kupata taarifa za kila siku. WHO inafanya kazi kwa karibu na wataalam wa kimataifa, serikali na wadau kupanua ujuzi wa kisayansi kuhusu virusi hivi vipya, kutokana na jinsi vinavyosambaa na athari zake na kutoa ushauri kwa nchi na watu, kuhusu hatua za kuchukua kwa ajili ya kulinda afya na kuzuia kuenea kwa mlipuko.
Taarifa kuhusu Virusi vya Corona
COVIDI-19 yazua changamoto za kupata huduma za afya Uganda
Kuendelea kusambaa kwa virusi vya Corona, COVID-19 kumezifanya nchi kukaza uzi zaidi katika hatua za kukabiliana na mlipuko huo ikiwemo vikwazo vya watu kutembea na hatua za kuwataka kusalia majumbani. Vikwazo hivi pamoja na kusaidia kudhibiti mlipuko wa COVID-19 lakini pia vimezua changamoto zingine. Mathalani nchini Uganda ambako kuna marufuku ya watu kutembea wagonjwa wengi wameanza kupata changamoto ya kufikia huduma za afya kutokana na maagizo mapya yanayolenga kudhibiti kuenea kwa virusi hivyo kama alivyobaini mwandishi wetu nchini humo John Kibego katika makala hii
Mashabiki wa mpira wa miguu duniani kote tuunde timu moja dhidi ya COVID-19-WHO na FIFA
Shirikisho la soka ulimwewnguni FIFA limeungana na Shirika la afya la Umoja wa Mataifa WHO katika kuunga mkono kampeni ya #BeActive yaani #Jishughulishe iliyozinduliwa leo katika Siku ya kimataifa ya Umoja wa Mataifa ya michezo kwa ajili ya maendeleo na amani ili kuhamasisha watu kuwa na afya wakiwa nyumbani wakati huu ambao dunia inaungana katika mapambano dhidi ya virusi vya corona, COVID-19, leo na kila siku.
Ubaguzi kwenye utoaji huduma dhidi ya COVID-19 utaleta janga zaidi- Wataalamu
Kikosi kazi cha waatalamu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa kuhusu watu wenye asili ya Afrika, kimetaka kuwepo na uwiano na usawa wa makundi mbalimbali ya binadamu wakati wa utoaji wa huduma kwa wagonjwa wa virusi vya Corona, COVID-19, la sivyo utoaji wa huduma kwa misingi ya rangi unaweza kusababisha vifo zaidi.
Jumuiya ya michezo yakabiliwa na changamoto kubwa sababu ya COVID-19 :UN
Ikiwa leo ni siku ya kimataifa ya michezo kwa maendeleo na amani , Umoja wa Mataifa umesema jumuiya ya kimataifa ya michezo inakabiliwa na changamoto kubwa wakati huu wa mlipuko wa virusi vya Corona, COVID-19 kwa watu wengi kushindwa kujumuika katika michezo mbalimbali na pia kufanya mazoezi.