Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Taarifa kuhusu Virusi vya Corona

Virusi vya Corona kama dharura ya afya ya umma:Taarifa za UN News Kiswahili
Mlipuko uliripotiwa mara ya kwanza Wuhan China Desemba 31, 2019

Ukurasa huu unaleta pamoja taarifa kuhusu muongozo kutoka kwa Shirika la afya la Umoja wa Mataifa, WHO na Umoja wa Mataifa kuhusu mlipuko wa sasa wa virusi vya corona au COVID-19, ambavyo viliripotiwa mara ya kwanza Wuhan, China mnamo Desemba 31, 2019. Tafadhali tembelea ukurasa huu kupata taarifa za kila siku. WHO inafanya kazi kwa karibu na wataalam wa kimataifa, serikali na wadau kupanua ujuzi wa kisayansi kuhusu virusi hivi vipya, kutokana na jinsi vinavyosambaa na athari zake  na kutoa ushauri kwa nchi na watu, kuhusu hatua za kuchukua kwa ajili ya kulinda afya na kuzuia kuenea kwa mlipuko.

Mtaa wa mabanda wa Mathare, jijini Nairobi, Kenya.
© Julius Mwelu/ UN-Habitat

Kenya yachukua hatua zaidi kudhibiti COVID-19, wakati wagonjwa wawili wakipona na wapya kuzuka

Wagonjwa wawili ambao wamethibitishwa kupona virusi vya corona nchini Kenya wameonekana hadharani kwa mara ya kwanza leo wakati wakizungumza kwa njia ya video na Rais Uhuru Kenyatta na kuonyeshwa kwenye runinga kadhaa nchini Kenya. Hata hivyo wizara ya afya nchini Kenya imatangaza kuwepo kwa wagonjwa 22 zaidi wa virusi vya corana hii leo na kufanya idadi jumla kufikia wagonjwa 81. 

Sauti
3'31"