Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Taarifa kuhusu Virusi vya Corona

Virusi vya Corona kama dharura ya afya ya umma:Taarifa za UN News Kiswahili
Mlipuko uliripotiwa mara ya kwanza Wuhan China Desemba 31, 2019

Ukurasa huu unaleta pamoja taarifa kuhusu muongozo kutoka kwa Shirika la afya la Umoja wa Mataifa, WHO na Umoja wa Mataifa kuhusu mlipuko wa sasa wa virusi vya corona au COVID-19, ambavyo viliripotiwa mara ya kwanza Wuhan, China mnamo Desemba 31, 2019. Tafadhali tembelea ukurasa huu kupata taarifa za kila siku. WHO inafanya kazi kwa karibu na wataalam wa kimataifa, serikali na wadau kupanua ujuzi wa kisayansi kuhusu virusi hivi vipya, kutokana na jinsi vinavyosambaa na athari zake  na kutoa ushauri kwa nchi na watu, kuhusu hatua za kuchukua kwa ajili ya kulinda afya na kuzuia kuenea kwa mlipuko.

Wakimbizi wa ndani walio katika jimbo la Kasai nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, DRC
© UNFPA DRC

Haki na afya ya wakimbizi, wahamiaji na wasio na utaifa inatakiwa kulindwa wakati wa kushughulikia COVID-19

Taarifa ya pamoja kwa vyombo vya habari iliyotolewa hii leo na Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa OHCHR, pamoja na mashirika ya Umoja wa Mataifa lile la wahamiaji, IOM, la kuhudumia wakimbizi UNHCR na la afya WHO imetoa wito kwa dunia kulinda haki na afya ya wakimbizi, wahamiaji na wasio na utaifa katika wakati huu wa mapambano dhidi ya virusi vya corona, COVID-19.

UN News/ John Kibego

COVID-19: Kutembea usiku sasa ni hatia Uganda

Uganda imefuata nyayo ya baadhi ya nchi duniani ya kupitisha amri ya kutotembea usiku kama mojawapo ya njia za kuzuia kuenea kwa ugonjwa wa virusi vya Corona, au COVID-19, sanjari na kufunga mipaka yake na kupiga marufuku usafiri wa magari binafsi. Haya hapa  maelezo zaidi na mwandishi wetu wa Uganda, John Kibego.

(Taarifa ya John Kibego)

Rais Yoweri Kaguta Museveni ametangaza maagizo mapya mapya kabisa kwa madhumuni ya kuzuia kusambaa zaidi kwa virusi hivyo nchini Uganda.

Sauti
2'9"
UN Photo/Loey Felipe

Kampuni ya ZuRi Africa yajitosa kusaidia harakati dhidi ya COVID-19 Tanzania

Kutokana na kuendelea kusambaa kwa virusi vya ugonjwa wa Corona, COVID-19, maeneo mbalimbali duniani, Umoja wa Mataifa umekuwa ukisihi wadau kujitokeza kuunga mkono hatua za kimataifa na kitaifa za kudhibiti kusambaa kwa virusi hivyo visivyo na tiba wala chanjo. Wito huo umeitikiwa vyema nchini Tanzania ambako kampuni binafsi zimejitokeza kuunga mkono serikali na miongoni mwao ni ile ya ZuRi Africa. Je wao wamefanya nini?

Sauti
4'15"
Bendera za Umoja wa Mataifa na ile ya Olimpiki zikiwa zinapepea kwa pamoja kwenye Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa
UN/Eskinder Debebe

COVID-19 yasababisha Olimpiki kusogezwa mwaka mmoja mbele, sasa kuchezwa 2021

Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki IOC na Kamati ya kimataifa ya Paralimpiki IPC au Olimpiki ya watu wenye ulemavu, kwa pamoja kamati ya maandalizi ya Tokyo 2020, Serikali ya mji wa Tokyo na serikali ya Japani wametangaza kuwa kutokana na mlipuko wa virusi vya Corona, COVID-19, sasa michezo ya Olimpiki iliyokuwa ifanyike mwaka huu mjini Tokyo, itafanyika mwaka ujao wa 2021.

Sauti
3'24"