Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Taarifa kuhusu Virusi vya Corona

Virusi vya Corona kama dharura ya afya ya umma:Taarifa za UN News Kiswahili
Mlipuko uliripotiwa mara ya kwanza Wuhan China Desemba 31, 2019

Ukurasa huu unaleta pamoja taarifa kuhusu muongozo kutoka kwa Shirika la afya la Umoja wa Mataifa, WHO na Umoja wa Mataifa kuhusu mlipuko wa sasa wa virusi vya corona au COVID-19, ambavyo viliripotiwa mara ya kwanza Wuhan, China mnamo Desemba 31, 2019. Tafadhali tembelea ukurasa huu kupata taarifa za kila siku. WHO inafanya kazi kwa karibu na wataalam wa kimataifa, serikali na wadau kupanua ujuzi wa kisayansi kuhusu virusi hivi vipya, kutokana na jinsi vinavyosambaa na athari zake  na kutoa ushauri kwa nchi na watu, kuhusu hatua za kuchukua kwa ajili ya kulinda afya na kuzuia kuenea kwa mlipuko.

UN News/ Stella Vuzo

Elimu kwa jamii kuhusu kuzuia kuenea kwa virusi vya corona Tanzania

Wakati ulimwengu unaendelea na mapambano dhidi ya virusi vya corona, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF linaeleza wasiwasi wake kuhusu elimu ya watoto kutokana na ulazima wa kufungwa kwas hule katika mataifa takribani 120 hivi sasa duniani kote. Shirika hilo linasema zaidi ya nusu ya wanafunzi wote ulimwenguni wameathiriwa na hatua ya kufungwa kwa shule ikiwa ni sehemu ya juhudi za kutokomeza ugonjwa huo.

Sauti
4'5"
Mtazamo wa maeneo ya forodhani visiwani Zanzibar.
UN News/Assumpta Massoi

COVID-19: Zanzibar yachukua hatua kupunguza mlundikano magerezani

Idadi ya wagonjwa wa virusi vya Corona, huko visiwani Zanzibar nchini Tanzania ikiwa imefikia wagonjwa wawili, hii leo serikali ya Mapinduzi Zanzibar imetangaza hatua za kuhakikisha sekta ya mahakama inaunga mkono hatua za kudhibiti kuenea kwa virusi vya Corona, COVID-19 ikiwemo kusitisha kwa muda usikilizaji wa kesi za madai na jinai. Omar Abdalla wa Televisheni washirika ZenjFM  kutoka Zanzibar ametuandalia taarifa hii.

Sauti
2'47"