Ukurasa huu unaleta pamoja taarifa kuhusu muongozo kutoka kwa Shirika la afya la Umoja wa Mataifa, WHO na Umoja wa Mataifa kuhusu mlipuko wa sasa wa virusi vya corona au COVID-19, ambavyo viliripotiwa mara ya kwanza Wuhan, China mnamo Desemba 31, 2019. Tafadhali tembelea ukurasa huu kupata taarifa za kila siku. WHO inafanya kazi kwa karibu na wataalam wa kimataifa, serikali na wadau kupanua ujuzi wa kisayansi kuhusu virusi hivi vipya, kutokana na jinsi vinavyosambaa na athari zake na kutoa ushauri kwa nchi na watu, kuhusu hatua za kuchukua kwa ajili ya kulinda afya na kuzuia kuenea kwa mlipuko.
Taarifa kuhusu Virusi vya Corona
IMF yatabiri mdororo wa uchumi duniani kufikia kiwango cha mwaka 2008 lakini kukwamuka mwaka 2021
Shirika la fedha duniani, IMF limesisitiza umuhimu wa hatua za pamoja duniani na mshikamano baina ya nchi zote katika vita dhidi ya ugonjwa wa virusi vya Corona, COVID-19 huku likisema kuwa mdororo wa uchumi kutokana na janga la sasa utafikia ule wa mwaka 2008 lakini matarajio ya kukwamuka ni mwakani.
Uganda sasa ina wagonjwa 8 wa COVID-19, masoko yote yafungwa
Nchini Uganda serikali imeimarisha juhudi za kudhibiti virusi vya Corona COVID-19 baada ya kuthibitishwa kwa wagonjwa wapya wanane katika nchi hiyo na kuwaacha wananchi wakiwa katika hali ya taharuki. Miongoni mwa hatua mpya zilizochukuliwa sasa ni uamuzi wa kufunga masoko ambayo yalikuwa yameaachwa wazi na kusababisha bei za bidhaa muhimu kupanda.
TB ikichanganyika na COVID-19 ni janga juu ya janga
Ugonjwa wa Kifua Kikuu au TB, bado umesalia kuwa miongoni mwa magonjwa hatari zaidi duniani. Zaidi ya watu 4000 hupoteza maisha yao kila siku kutokana na ugonjwa TB huku 30,000 wakiwa wanapata maambukizi ya ugonjwa huu unaoweza kuzuiwa na kutibiwa. Gonjwa hili linasalia kuwa tishio wakati huu ambapo kumeibuka virusi vya ugonjwa wa Corona au COVID-19 ambao nao umetikisa dunia ukisambaa katika mataifa 189 na ukiwa umesababisha vifo vya watu zaidi ya 14,500 tangu kubainika mwezi Desemba mwaka jana.
OHCHR yataka vikwazo ziondolewe kusaidia wagonjwa wa COVID-19
Wakati idadi ya wagonjwa wa virusi vya Corona, COVID-19 ulimwenguni ikizidi kupaa na kuwa zaidi ya 330,000 huku vifo vikifikia 1,4652, Kamishna Mkuu wa haki za binadamu, Michelle Bachelet ametaka vikwazo vya kisekta duniani viondolewe ili mataifa yaweza kukabiliana na mlipuko wa virusi hivyo. Grace Kaneiya na ripoti kamili.
(Taarifa ya Grace Kaneiya)
Uwepo wa COVID-19 usitufanye tusahau kuhusu tishio la TB
Tunapopambana na janga la kimataifa la afya COVID-19 ni wakati pia wa kutafakari na kutoyapa kisogo maradhi mengine makubwa ikiwemo kifua kikuu au TB, amesema mkurugenzi mkuu wa shirika la afya duniani WHO. Flora Nducha na taarifa zaidi
(TAARIFA YA FLORA NDUCHA)
Mkurugenzi huyo Dkt. Tedros Adhamon Ghebreyesus ameikumbusha dunia na kila mtu kwamba ingawa virusi vya corona, COVID-19 ndio vinavyogonjwa vichwa vya habari kila kona ya dunia kuna gonjwa lingine la mfumo wa hewa ambalo ni chagamoto kwa dunia
24 Machi 2020
Assumpta Massoi : Hujambo na Karibu kusikiliza Jarida kutoka Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa, kutoka hapa New York Marekani.
JINGLE (04”)
ASSUMPTA:Ni jumanne ya Machi Ishirini na nne mwaka 2020, mwenyeji wako studioni hii leo ni mimi ASSUMPTA MASSOI
Ondoeni vikwazo kusaidia COVID-19, madaktari wasemao ukweli msiwaadhibu- Bachelet
Wakati idadi ya wagonjwa wa virusi vya Corona, COVID-19 ulimwenguni ikizidi kupaa na kuwa zaidi ya 330,000 huku vifo vikifikia 14,652 Kamishna Mkuu wa haki za binadamu, Michelle Bachelet ametaka vikwazo vya kisekta duniani viondolewe ili mataifa yaweza kukabiliana na mlipuko wa virusi hivyo.
Tunapopambana na COVID-19 tusiyape kisogo maradhi kama TB:WHO
Tunapopambana na janga la kimataifa la afya COVID-19 ni wakati pia wa kutafakari na kutoyapa kisogo maradhi mengine makubwa ikiwemo kifua kikuu au TB, amesema mkurugenzi mkuu wa shirika la afya duniani WHO.