Virusi vya Corona kama dharura ya afya ya umma:Taarifa za UN News Kiswahili
Mlipuko uliripotiwa mara ya kwanza Wuhan China Desemba 31, 2019

Ukurasa huu unaleta pamoja taarifa kuhusu muongozo kutoka kwa Shirika la afya la Umoja wa Mataifa, WHO na Umoja wa Mataifa kuhusu mlipuko wa sasa wa virusi vya corona au COVID-19, ambavyo viliripotiwa mara ya kwanza Wuhan, China mnamo Desemba 31, 2019. Tafadhali tembelea ukurasa huu kupata taarifa za kila siku. WHO inafanya kazi kwa karibu na wataalam wa kimataifa, serikali na wadau kupanua ujuzi wa kisayansi kuhusu virusi hivi vipya, kutokana na jinsi vinavyosambaa na athari zake  na kutoa ushauri kwa nchi na watu, kuhusu hatua za kuchukua kwa ajili ya kulinda afya na kuzuia kuenea kwa mlipuko.

Kwenye vita watu milioni 100 wako hatarini kwa COVID-19:OCHA

Wakati virusi vya Corona , COVID-19 vikiendelea kusambaa kote duniani Umoja wa Mataifa unatiwa hofu kuhusu athari kwa watu milioni 100 wanaoishi katika maeneo ya vita na dharura nyingine ambao wanategemea misaada ya kibinadamu.

Harakati za kuzuia kusambaa kwa COVID-19 huenda zikawaweka wanawake hatarini ya ukatili -UN Women

Wakati janga la ugonjwa wa virusi vya Corona, au COVID-19 likiendelea kutikisa duniani, shirika la Umoja wa Mataifa la kushughulikia masuala ya wanawake, UN Women linashirikiana na wadau wake kuhakikisha kuwa madhara ya ugonjwa huo katika jinsia yanaepukika. Grace Kaneiya na ripoti kamili.

Sauti -
2'24"

Hisia za wakimbizi nchini Uganda kufuatia mlipuko wa Corona unaoshuhudiwa duniani kote

Katika makala ya wiki hii tutakuwa nchini Uganda tukiangazia shaka na shuku miongoni mwa wakimbizi na hatua za Umoja wa Mataifa wakati huu wa maambukizi ya Corona.  

Sauti -
4'56"

Mahitaji ya wanawake yapatiwe kipaumbele wakati wa COVID-19: UN Women

Wakati janga la ugonjwa wa virusi vya Corona, au COVID-19 likiendelea kutikisa duniani, shirika la Umoja wa Mataifa la kushughulikia masuala ya wanawake, UN Women linashirikiana na wadau wake kuhakikisha kuwa madhara ya ugonjwa huo katika jinsia yanaepukika.