Virusi vya Corona kama dharura ya afya ya umma:Taarifa za UN News Kiswahili
Mlipuko uliripotiwa mara ya kwanza Wuhan China Desemba 31, 2019

Ukurasa huu unaleta pamoja taarifa kuhusu muongozo kutoka kwa Shirika la afya la Umoja wa Mataifa, WHO na Umoja wa Mataifa kuhusu mlipuko wa sasa wa virusi vya corona au COVID-19, ambavyo viliripotiwa mara ya kwanza Wuhan, China mnamo Desemba 31, 2019. Tafadhali tembelea ukurasa huu kupata taarifa za kila siku. WHO inafanya kazi kwa karibu na wataalam wa kimataifa, serikali na wadau kupanua ujuzi wa kisayansi kuhusu virusi hivi vipya, kutokana na jinsi vinavyosambaa na athari zake  na kutoa ushauri kwa nchi na watu, kuhusu hatua za kuchukua kwa ajili ya kulinda afya na kuzuia kuenea kwa mlipuko.

Pamoja na kujitenga na kufunga shule tuongeze juhudi za upimaji COVID-19:WHO

Wakati virusi vya corona vikiendelea kusambaa sehemu mbalimbali duniani na kuongeza idadi ya vifo, shirika la afya ulimwenguni WHO linasema huu ni wakati wa kuongeza kasi ya upimaji.

Wagonjwa wa Corona duniani sasa wavuka 153,000, Tanzania nayo imo

Idadi ya wagonjwa wa Corona duniani ikivuka 153,000,  wataalam wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa katika taarifa yao iliyotolewa leo mjini Geneva Uswisi wamezitaka nchi kuepuka kutumia mbinu za kudhibiti mlipuko zinazokandamiza haki za binadamu.

Hatua za dharura dhidi ya COVID-19 zisitumike kubinya haki za binadamu: UN

Wataalamu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa wamezitaka nchi kuhakikisha kwamba hawazitumii vibaya hatua za dharura za kukabiliana na mlipuko wa virusi vya Corona, COVID-19 kwa kubinya haki za binadamu.