Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Taarifa kuhusu Virusi vya Corona

Virusi vya Corona kama dharura ya afya ya umma:Taarifa za UN News Kiswahili
Mlipuko uliripotiwa mara ya kwanza Wuhan China Desemba 31, 2019

Ukurasa huu unaleta pamoja taarifa kuhusu muongozo kutoka kwa Shirika la afya la Umoja wa Mataifa, WHO na Umoja wa Mataifa kuhusu mlipuko wa sasa wa virusi vya corona au COVID-19, ambavyo viliripotiwa mara ya kwanza Wuhan, China mnamo Desemba 31, 2019. Tafadhali tembelea ukurasa huu kupata taarifa za kila siku. WHO inafanya kazi kwa karibu na wataalam wa kimataifa, serikali na wadau kupanua ujuzi wa kisayansi kuhusu virusi hivi vipya, kutokana na jinsi vinavyosambaa na athari zake  na kutoa ushauri kwa nchi na watu, kuhusu hatua za kuchukua kwa ajili ya kulinda afya na kuzuia kuenea kwa mlipuko.

Unsplash/Aalok Atreya

Baada ya mgonjwa wa Corona kuthibitishwa Kenya, mikusanyiko mikubwa yapigwa marufuku

Nchini Kenya kufuatia kuthibitishwa kwa mgonjwa wa kwanza wa virusi vya Corona, COVID-19, shirika la afya ulimwenguni WHO nchini humo limesema linashirikiana na serikali katika hatua zote za kudhibiti kusambaa kwa virusi hivyo katika taifa hilo la Afrika Mashariki, wakati huu ambapo mgonjwa huyo amewekwa katika karantini kwenye hospitali  ya Kenyatta jijini Nairobi hadi pale atakapobainika kuwa hana tena virusi.

Sauti
3'48"
Picha iliyotengenezwa kidijitali ikionesha maambukizi ya kirusi cha corona katka rangi ya buluu, kisa cha kwanza kilichogundulika Marekani
CDC/Hannah A Bullock/Azaibi Tami

Mgonjwa wa Corona nchini Kenya alirejea nyumbani kutokea Marekani akipitia Uingereza

Nchini Kenya kufuatia kuthibitishwa kwa mgonjwa wa kwanza wa virusi vya Corona, COVID-19, shirika la afya ulimwenguni WHO nchini humo limesema linashirikiana na serikali katika hatua zote za kudhibiti kusambaa kwa virusi hivyo katika taifa hilo la Afrika Mashariki, wakati huu ambapo mgonjwa huyo amewekwa katika karantini kwenye hospitali  ya Kenyatta jijini Nairobi hadi pale atakapobainika kuwa hana tena virusi.

Sauti
3'48"

13 Machi 2020

Nchini Kenya kufuatia kuthibitishwa kwa mgonjwa wa kwanza wa virusi vya Corona, COVID-19, shirika la afya ulimwenguni WHO nchini humo limesema linashirikiana na serikali katika hatua zote za kudhibiti kusambaa kwa virusi hivyo katika taifa hilo la Afrika Mashariki. Aibu ya kurejea nyumbani mikono mitupu inatuponza, wasema wahamiaji. Programu ya kuimarisha stadi yasaidia mkimbizi kutoka Colombia kufikia ndoto zake.

Sauti
9'40"