Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Taarifa kuhusu Virusi vya Corona

Virusi vya Corona kama dharura ya afya ya umma:Taarifa za UN News Kiswahili
Mlipuko uliripotiwa mara ya kwanza Wuhan China Desemba 31, 2019

Ukurasa huu unaleta pamoja taarifa kuhusu muongozo kutoka kwa Shirika la afya la Umoja wa Mataifa, WHO na Umoja wa Mataifa kuhusu mlipuko wa sasa wa virusi vya corona au COVID-19, ambavyo viliripotiwa mara ya kwanza Wuhan, China mnamo Desemba 31, 2019. Tafadhali tembelea ukurasa huu kupata taarifa za kila siku. WHO inafanya kazi kwa karibu na wataalam wa kimataifa, serikali na wadau kupanua ujuzi wa kisayansi kuhusu virusi hivi vipya, kutokana na jinsi vinavyosambaa na athari zake  na kutoa ushauri kwa nchi na watu, kuhusu hatua za kuchukua kwa ajili ya kulinda afya na kuzuia kuenea kwa mlipuko.

Washiriki wa CSW63 wakisherehekea kukamilika kwa mkutano huo mjini New York Marekani.
UN Women/Ryan Brown

Virusi vya Corona vyasababisha kuahirishwa kwa mkutano wa 64 wa CSW

Virusi vya Corona au COVID-19 vimeendelea kuathiri shughuli a kiuchumi, kijamii na kisiasa duniani na athari hasi za hivi karibuni zaidi ni kuahirishwa kwa mkutano wa 64 wa Kamisheni ya hali ya wanawake duniani, CSW uliokuwa ufanyike kwa wiki mbili hapa kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani kuanzia tarehe 9 hadi 20 mwezi huu wa Machi.

Sauti
2'18"

04 MACHI 2020

Elimu kwa wasichana haina maana iwapo jamii ina mtazamo hasi dhidi yao imesema ripoti ya mashirika ya Umoja wa Mataifa. Virusi vya Corona vyasababisha kuahirishwa kwa mkutano wa 64 wa CSW. Tunafanya kila tuwezalo kuwasaidia waathirika wa vita Idlib imesema WFP.

Sauti
11'28"