Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Taarifa kuhusu Virusi vya Corona

Virusi vya Corona kama dharura ya afya ya umma:Taarifa za UN News Kiswahili
Mlipuko uliripotiwa mara ya kwanza Wuhan China Desemba 31, 2019

Ukurasa huu unaleta pamoja taarifa kuhusu muongozo kutoka kwa Shirika la afya la Umoja wa Mataifa, WHO na Umoja wa Mataifa kuhusu mlipuko wa sasa wa virusi vya corona au COVID-19, ambavyo viliripotiwa mara ya kwanza Wuhan, China mnamo Desemba 31, 2019. Tafadhali tembelea ukurasa huu kupata taarifa za kila siku. WHO inafanya kazi kwa karibu na wataalam wa kimataifa, serikali na wadau kupanua ujuzi wa kisayansi kuhusu virusi hivi vipya, kutokana na jinsi vinavyosambaa na athari zake  na kutoa ushauri kwa nchi na watu, kuhusu hatua za kuchukua kwa ajili ya kulinda afya na kuzuia kuenea kwa mlipuko.

Watu wakiwa wamevalia vifaa vya kujikinga katika eneo la kusubiri katika uwanja wa ndege wa Shenzhen Bao'an wa kimataifa.
UN News/Jing Zhang

Tuko tayari kusaidia kiufundi katika mlipuko wa corona:IOM

Wakati hofu ikiendelea kutanda kuhusu idadi ya visa vilivyoripotiwa kutokana na mlipuko wa virusi vipya vya Corona na pia kusambaa kwake katika nchi 18 hivi sasa, shirika la umoja wa Mataifa la uhamiaji IOM limesema liko tayari kutoa msaada wa kiufundi kwa serikali likishirikiana na shirika la afya ulimwenguni WHO ili kuwawezesha watu kusafiri katika njia salama kiafya na kusaidia utekelezaji wa hatua za afya za kijamii ili kuhakikisha athari ndogo katika jamii na uchumi.

31 JANUARI 2020

Jaridani Januari 31, 2020 na Arnold Kayanda. Ikiwa leo ni Ijumaa utasikia Habari kwa ufupi, mada kwa kina imejikita katika mlipuko wa virusi vya corona tukiangazia nchini Kenya ambako kuna mgonjwa anayefanyiwa uchunguzi kuthibitisha iwapo ana virusi vya corona baada ya kuwasili kutoka China na dalili za homa. Na ikiwa leo ni Ijumaa tutasikia uchambuzi wa neno la wiki kutoka BAKITA.

Sauti
11'4"