Mabadiliko ya Tabianchi
Ujumbe kutoka kwa Katibu Mkuu

Lengo namba 13 la malengo ya maendeleo endelevu, SDGs linataka uhifadhi wa mazingira kwa kuchukua hatua muafaka. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio  Guterres akiwa ziarani katika nchi zilizoko ukanda wa pasifiki anapaza sauti ya kile kinachopaswa kufanywa kwa ubia ili kulinda sayari dunia kwa faida ya kizazi cha sasa na vizazi vijavyo.

Ni wakati wa kuacha kuikaanga sayari yetu na kutimiza ahadi za mabadiliko ya tabianchi kwa vitendo:Guterres

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres leo ameonya kwamba dunia inaelekea pabaya linapokuja suala la mabadiliko ya tabianchi , ni suala la aibu linaloambatana na ahadi hewa ambazo zinamuweka kila mtu kwenye hatari ya zahma kubwa.