Mabadiliko ya Tabianchi
Ujumbe kutoka kwa Katibu Mkuu

Lengo namba 13 la malengo ya maendeleo endelevu, SDGs linataka uhifadhi wa mazingira kwa kuchukua hatua muafaka. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio  Guterres akiwa ziarani katika nchi zilizoko ukanda wa pasifiki anapaza sauti ya kile kinachopaswa kufanywa kwa ubia ili kulinda sayari dunia kwa faida ya kizazi cha sasa na vizazi vijavyo.

COP26 ikifungua pazia WMO yasema miaka 7 iliyopita imevunja rekodi ya joto duniani

Miaka saba iliyopita inaelekea kuwa ya joto zaidi kuwahi kurekodiwa sanjari na kupanda kwa kina cha bahari ni katika viwango vya kuvunja rekodi, kulingana na ripoti ya muda ya shirika la hali ya hewa duniani (WMO) ya hali ya hewa duniani kwa mwaka 2021, iliyotolewa Jleo umapili, wakati mkutano wa Umoja wa Mataifa wa mabadiliko ya tabianchi COP26, ukifunguliwa Glasgow, Uingereza.

Tukiadhimisha siku ya miji tudhibiti hatari za mabadiliko ya tabianchi na kujenga mnepo:UN 

Leo ni siku ya miji duniani, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mastaifa amesema ingawa kupanda kwa kina cha bahari kunaweza kuweka zaidi ya watu milioni 800 katika miji ya pwani kwenye hatari ya moja kwa moja ifikapo mwaka 2050, chini ya asilimia 10 ya fedha za mabadiliko ya tabianchi kwa maeneo ya mijini zinakwenda katika hatua za kukabiliana na kujenga mnepo. 

COP26 – Tunachofahamu kwa sasa, na kwa nini ni muhimu: Muongozo wako wa habari kutoka Umoja wa Mataifa 

Katika dunia iliyotikiswa na mliipuko na kuwa dirisha lililofuga fursa za kupambana na majanga ya tabianchi, mkutano muhimu wa Umoja wa Mataifa wa COP26 unang’oa nanga leo Jumapili katika mji wa Glasgow nchini Scotland madhara ya janga hilo yasingekuwa makubwa zaidi kama yalivyo sasa.