Mabadiliko ya Tabianchi
Ujumbe kutoka kwa Katibu Mkuu

Lengo namba 13 la malengo ya maendeleo endelevu, SDGs linataka uhifadhi wa mazingira kwa kuchukua hatua muafaka. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio  Guterres akiwa ziarani katika nchi zilizoko ukanda wa pasifiki anapaza sauti ya kile kinachopaswa kufanywa kwa ubia ili kulinda sayari dunia kwa faida ya kizazi cha sasa na vizazi vijavyo.

Miji ni chachu ya vita dhidi ya mabadiliko ya tabianchi: Guterres 

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ametoa mifano kadhaa ya jinsi miji ambavyo tayari inafanikiwa katika hatua za kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi alipozungumza katika mkutano wa Kikundi cha C40 wa kundi la miji mikubwa ya Uongozi dhidi ya mabadiliko ya tabianchi, kwani katikati ya miji wameathirika zaidi na jangala corona au COVID-29, na viwango vya juu vya vifo na upotevu wa uchumi.