Mabadiliko ya Tabianchi
Ujumbe kutoka kwa Katibu Mkuu

Lengo namba 13 la malengo ya maendeleo endelevu, SDGs linataka uhifadhi wa mazingira kwa kuchukua hatua muafaka. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio  Guterres akiwa ziarani katika nchi zilizoko ukanda wa pasifiki anapaza sauti ya kile kinachopaswa kufanywa kwa ubia ili kulinda sayari dunia kwa faida ya kizazi cha sasa na vizazi vijavyo.

Uhusiano kati ya biashara yetu na mazingira ni wa ajabu sana-Wauza miche ya miti Tanzania

Biashara ya uuzaji wa miche ya miti nchini Tanzania hususani katika jiji la Dar es Salaam ni ya miaka mingi. Wauzaji wanasema ingawa uhusiano kati ya miti na mazingira ni  wa wazi mno, lakini kwao uhusiano huu ni wa ajabu.

Sauti -
3'30"