Mabadiliko ya Tabianchi
Ujumbe kutoka kwa Katibu Mkuu

Lengo namba 13 la malengo ya maendeleo endelevu, SDGs linataka uhifadhi wa mazingira kwa kuchukua hatua muafaka. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio  Guterres akiwa ziarani katika nchi zilizoko ukanda wa pasifiki anapaza sauti ya kile kinachopaswa kufanywa kwa ubia ili kulinda sayari dunia kwa faida ya kizazi cha sasa na vizazi vijavyo.

10 Machi 2020

Kuna ongezeko la ishara na madhara ya mabadiliko ya tabianchi katika anga, ardhi na baharini yasema ripoti ya WMO. Programu ya kupatia wakimbizi wa Syria fedha Uturuki yawa nguzo ya maisha yao. MINUSCA yawapatia wanawake wafungwa CAR mafunzo ya ujasiriamali.

Sauti -
10'26"

Ripoti mpya yaonesha kuna ongezeko la ishara na madhara ya mabadiliko ya tabianchi katika anga, ardhi na baharini

Ishara za mabadiliko ya tabianchi kama vile ongezeko la joto la ardhini na baharini, kuongezeka kwa kina cha bahari na kuyeyuka kwa barafu, vimeangaziwa katika ripoti mpya ya Shirika la utabiri wa hali ya hewa duniani WMO na wadau wake iliyotolewa hii leo Machi 10 mjini New York Marekani na Genev

Sauti -
2'29"