Mabadiliko ya Tabianchi
Ujumbe kutoka kwa Katibu Mkuu

Lengo namba 13 la malengo ya maendeleo endelevu, SDGs linataka uhifadhi wa mazingira kwa kuchukua hatua muafaka. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio  Guterres akiwa ziarani katika nchi zilizoko ukanda wa pasifiki anapaza sauti ya kile kinachopaswa kufanywa kwa ubia ili kulinda sayari dunia kwa faida ya kizazi cha sasa na vizazi vijavyo.

Hatua dhidi ya athari ya mabadiliko ya tabianchi Kenya

Dunia imeadhimisha siku ya familia Mei 15, mwaka huu ikibeba kaulimbiu familia na hatua katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

Sauti -
5'26"

Tuvalu nathamini jitihada zenu za mnepo dhidi ya mabadiliko ya tabianchi:Guterres

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema anathamini na kutiwa moyo na jitihada zinazofanywa na serikali ya kisiwa cha Tuvalu katika vita dhidi ya mabadiliko ya tabianchi.