Mabadiliko ya Tabianchi
Ujumbe kutoka kwa Katibu Mkuu

Lengo namba 13 la malengo ya maendeleo endelevu, SDGs linataka uhifadhi wa mazingira kwa kuchukua hatua muafaka. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio  Guterres akiwa ziarani katika nchi zilizoko ukanda wa pasifiki anapaza sauti ya kile kinachopaswa kufanywa kwa ubia ili kulinda sayari dunia kwa faida ya kizazi cha sasa na vizazi vijavyo.

Teknolojia ya asili ya wafugaji inasaidia mnepo wa mabadiliko ya tabianchi:TANIPE

Changamoto za mabadiliko ya tabianchi kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa hazichagui wala hazibagui taifa au jamii utokayo zinamuathiri kila mtu duniani na ndio maana wito unatolewa kila uchao kuchukua hatua zote stahiki kujenga mnepo dhidi ya zahma hiyo kote duniani.

Sauti -
5'15"