Mabadiliko ya Tabianchi
Ujumbe kutoka kwa Katibu Mkuu

Lengo namba 13 la malengo ya maendeleo endelevu, SDGs linataka uhifadhi wa mazingira kwa kuchukua hatua muafaka. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio  Guterres akiwa ziarani katika nchi zilizoko ukanda wa pasifiki anapaza sauti ya kile kinachopaswa kufanywa kwa ubia ili kulinda sayari dunia kwa faida ya kizazi cha sasa na vizazi vijavyo.

Katika mabadiliko ya tabianchi ujihadhari kabla ya shari ni muhimu:UNEP

Iki kukabiliana na athari kubwa za majanga yanayochangiwa na mabadiliko ya tabianchi ni muhimu kujihadhari kabla ya shari kwa maandalizi muafa limesema shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa mazingira UNEP.

Sauti -
5'37"

Japo majanga mengine hayaepukiki, tahadhari ni muhimu:UNEP

Hivi karibuni katika maeneo mengi ya Afrika Mashariki hali ya joto la kupindukia, mafuriko na kuchelewa au kukosekana kwa mvua imekuwa ni gumzo kubwa huku wakulima wakihaha kuokoa mazao yao.