Mabadiliko ya Tabianchi
Ujumbe kutoka kwa Katibu Mkuu

Lengo namba 13 la malengo ya maendeleo endelevu, SDGs linataka uhifadhi wa mazingira kwa kuchukua hatua muafaka. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio  Guterres akiwa ziarani katika nchi zilizoko ukanda wa pasifiki anapaza sauti ya kile kinachopaswa kufanywa kwa ubia ili kulinda sayari dunia kwa faida ya kizazi cha sasa na vizazi vijavyo.

Mazao yaliyotelekezwa sasa kugeuka mkombozi wa njaa:FAO 

Katika historia ya mwandamu, kati ya aina 30,000 za mimea , ni aina 6000 hadi 7000 pekee ndizo zimekuwa zikilimwa kwa ajili ya chakula kufikia leo hii , na ni takriban aina 170 tu za mazao ndio zinatumika kwa kiwango kikubwa katika biashara , kwa mujibu wa ripoti ya shirika la chakula na kilimo FAO iliyotolewa juma hili.