Mabadiliko ya Tabianchi
Ujumbe kutoka kwa Katibu Mkuu

Lengo namba 13 la malengo ya maendeleo endelevu, SDGs linataka uhifadhi wa mazingira kwa kuchukua hatua muafaka. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio  Guterres akiwa ziarani katika nchi zilizoko ukanda wa pasifiki anapaza sauti ya kile kinachopaswa kufanywa kwa ubia ili kulinda sayari dunia kwa faida ya kizazi cha sasa na vizazi vijavyo.

Tusipotunza mazingira, hayatatutunza- Maloba

Utunzaji wa mazingira ni suala ambalo linahitaji ushiriki wa kila mtu kwani 'tusipotunza mazingira, hayatatutunza.' Hayo yamesemwa na Innocent Maloba kutoka shirika la World Wide Fund kwa ajili ya mazingira linalofanya kazi katika takriban nchi mia moja kote duniani. 

Sauti -
4'34"

Kupunguza hasara za kiuchumi zitokanazo na majanga kutabadili maisha:UN

Kuweza kupungunza hasara za kiuchumi zitokanazo na majanga ynayochangiwa na mabadiliko ya tabia nchi  kutasaidia kubadili maisha ya mamilioni ya watu umesema Umoja wa Mataifa.