Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UDHR70

UDHR70
Tamko la Haki za Binadamu la UN-Uchambuzi wa Ibara

Tamko la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa, UDHR, ni nyaraka ya kihistoria iliyopitishwa na nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa mwaka 1948 kwa lengo la kuhakikisha haki za binadamu zinalindwa. Rasimu ya nyaraka hii iliandaliwa na wawakilishi wenye usuli tofauti kuanzia sheria hadi utamaduni na walitoka maeneo yote ya dunia. Baada ya kuiandaa na kuijadili rasimu hiyo ilipitishwa na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa tarehe 10 Disemba mwaka 1948 mjini Paris, Ufaransa kwa azimio namba 217 A la baraza hilo. Likipatiwa jina la tamko la haki za binadmu, nyaraka hiyo inaweka viwango vya pamoja vya haki za binadamu kwa wote na mataifa yote. Azimio hilo, kwa mara ya kwanza liliweka misingi ya haki za binadamu inayokubalika kimataifa na inayopaswa kulindwa popote pale duniani. Hadi sasa nyaraka hiyo imetafsiriwa kwa zaidi ya lugha 500 ikiwemo Kiswahili.

Pata taarifa kila wakati pindi tunapochapisha taarifa mpya kwa kujisajili

UN/Eskinder Debebe

Utamaduni wa jamii yako ni haki  yako, lasema tamko la haki za binadamu la UN

Katika mwendelezo wa uchambuzi wa ibara kwa ibara za tamko la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa leo tunamulika ibara ya 27 inayosema kuwa kila mtu ana haki ya kushiriki na kunufaika na tamaduni, sanaa na sayansi ya jamii yake. Hii imenyumbuliwa katika pande mbili ambapo ili kuweza kupata ufafanuzi wa kisheria Grace Kaneiya wa Idhaa hii amezungumza na Dkt. Elifuraha Laltaika, mhadhiri wa sheria kutoka Chuo Kikuu cha Tumaini Makumira nchini Tanzania na anaanza kwa kufafanua yaliyomo.

 

Sauti
2'2"
Mtafiti Rebecca Adami akiwa katika studio za UN News kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York Marekani.
UN News/Paulina Greer

Wanawake walikuwa na mchango mkubwa katika kuandikwa kwa tamko la haki za binadamu

Wiki ijayo, dunia itaadhimisha miaka 70 ya tamko la Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu. Ingawa historia ya dunia inaonekana kuwasahau wanawake, mtafiti wa masuala ya haki za binadamu Dkt Rebecca Adami katika kitabu chake cha ‘Wanawake na tamko la haki za binadamu’ anasema wanawake walikuwa na mchango mkubwa katika kuliandaa na kulitekeleza tamko hilo.