Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UDHR70

UDHR70
Tamko la Haki za Binadamu la UN-Uchambuzi wa Ibara

Tamko la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa, UDHR, ni nyaraka ya kihistoria iliyopitishwa na nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa mwaka 1948 kwa lengo la kuhakikisha haki za binadamu zinalindwa. Rasimu ya nyaraka hii iliandaliwa na wawakilishi wenye usuli tofauti kuanzia sheria hadi utamaduni na walitoka maeneo yote ya dunia. Baada ya kuiandaa na kuijadili rasimu hiyo ilipitishwa na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa tarehe 10 Disemba mwaka 1948 mjini Paris, Ufaransa kwa azimio namba 217 A la baraza hilo. Likipatiwa jina la tamko la haki za binadmu, nyaraka hiyo inaweka viwango vya pamoja vya haki za binadamu kwa wote na mataifa yote. Azimio hilo, kwa mara ya kwanza liliweka misingi ya haki za binadamu inayokubalika kimataifa na inayopaswa kulindwa popote pale duniani. Hadi sasa nyaraka hiyo imetafsiriwa kwa zaidi ya lugha 500 ikiwemo Kiswahili.

Pata taarifa kila wakati pindi tunapochapisha taarifa mpya kwa kujisajili

UNICEF/UN0153963/Obadi

Mkimbizi bila elimu ni sawa na mti bila matunda:Mkimbizi Rachel

Elimu kwa mkimbizi ni muhimu sana, kwani bila elimu huwezi fanya chochote , iwe ni kwa upande wa ajira au hata ujasiriliamali, unakuwa sawa na mti usiozaa matunda ambao huonekana kutokuwa na faida yoyote. Kauli hiyo ni ya mmoja wa wakimbizi kutoka Jamhuri ya Kidekrasia ya Congo DRC, ambaye aliishi na kusomea kambini nchini Uganda. Akizungumza na mwandishi wetu John Kibego kuhusu haki ya kila mtu kupata elimu bila kujali kabila, rangi au uraia wake kama ilivyoainishwa kwenye Ibara ya 26 ya tamko la haki za binadamu, anasema haijalishi mazingira uliyopo “elimu ni elimu”.

Sauti
3'32"