Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UDHR70

UDHR70
Tamko la Haki za Binadamu la UN-Uchambuzi wa Ibara

Tamko la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa, UDHR, ni nyaraka ya kihistoria iliyopitishwa na nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa mwaka 1948 kwa lengo la kuhakikisha haki za binadamu zinalindwa. Rasimu ya nyaraka hii iliandaliwa na wawakilishi wenye usuli tofauti kuanzia sheria hadi utamaduni na walitoka maeneo yote ya dunia. Baada ya kuiandaa na kuijadili rasimu hiyo ilipitishwa na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa tarehe 10 Disemba mwaka 1948 mjini Paris, Ufaransa kwa azimio namba 217 A la baraza hilo. Likipatiwa jina la tamko la haki za binadmu, nyaraka hiyo inaweka viwango vya pamoja vya haki za binadamu kwa wote na mataifa yote. Azimio hilo, kwa mara ya kwanza liliweka misingi ya haki za binadamu inayokubalika kimataifa na inayopaswa kulindwa popote pale duniani. Hadi sasa nyaraka hiyo imetafsiriwa kwa zaidi ya lugha 500 ikiwemo Kiswahili.

Pata taarifa kila wakati pindi tunapochapisha taarifa mpya kwa kujisajili

Nchi zinatakiwa kubadili sheria zao ili kwenda sawa na mbinu za sasa za utumwa na utwana.

Ibara ya 4 ya tamko la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa linalotimiza miaka 70 mwaka huu wa 2018, inaeleza kinagaubaga kuwa hakuna mtu anayestahili kugeuzwa mtumwa na wala kuwa mtwana wa mtu yeyote. Na ingawa kwa miaka mingi nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa zimeridhia na pia kutunga sheria za kuunga mkono ibara hii, mabadiliko ya namna utumwa na utwana unavyotafsiriwa yaneziacha nyuma sheria nyingi. Wakili Jebra Kambole wa Tanzania katika mazungumzo haya na Arnold Kayanda, anasema kuna haja ya jumuiya ya kimataifa kulitizamasuala hili kwa namna mpya.

Sauti
2'51"