Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

Habari Mpya

WFP yajiandaa kukabili njaa baada ya kura ya maoni Sudan

Wakati Sudan Kusini inajiandaa kupiga kura ya maoni mwishoni mwa wiki hii, shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula WFP linajitahidi kuhakikisha kura hiyo ya kihistoria haita changia njaa zaidi katika eneo hilo ambalo limeghubikwa na miongo ya vita na majanga ya asili.

Haki za wapiga kura ziheshimiwe Sudan:Navi Pillay

Zikiwa zimesalia siku mbili kabla ya wananchi wa Sudan Kusini kuanza kupiga kura ya maoni ya kuamua hatma yao hapo siku ya Jumapili ijayo, mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Navi Pillay ameutaka uongozi wa Sudan kuhakikisha kura ya maoni inakuwa huru na ya haki.

Ouattara amkataka Gbagbo kukubali kushinda

Mgombea wa upinzani aliyetangazwa mshindi katika uchaguzi wa Novemba mwaka jana na kuzua utata nchini Ivory Coast Alassane Ouattara amesema ana imani suluhu ya mzozo wa kisiasa nchini humo itapatikana hivi karibuni.