Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

Habari Mpya

Mmoja wa Raia wa Uganda akipokea chanjo yake ya kwanza ya Covid-19 huko Hoima, Uganda.
John Kibego

Uganda yashirikiana na sekta binafsi kufikisha chanjo dhidi ya COVID-19 kwa wananchi 

Ili kuudhibiti ugonjwa wa Covid-19 unaosababishwa na virusi vya Corona, serikali ya Uganda imeamua kushirikiana zaidi na wadau mbalimbali yakiwemo makampuni ya mawasiliano na yale ya vinywaji katika juhudi za kuimarisha chanjo.  Je, kampeni hiyo inatekelezwaje? Na mtazamo wa Waganda kuhusu chanjo hiyo ukoje sasa? Hii hapa taarifa iliyoandaliwa na mwandishi wetu wa Uganda John Kibego.

Katibu Mkuu  António Guterres ametembelea maonesho ya picha ya "Mikononi mwao: Wanawake wachukua umiliko wa amani" katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa
UN Photo/Mark Garten)

Muda wa kurudisha nyuma saa ya haki za wanawake umepita, sasa iende mbele- Guterres alieleza Baraza

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa leo limekuwa na mjadala wa wazi kuhusu wanawake, amani na usalama ambapo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema wakati umefika kwa baraza hilo kuonesha kwa vitendo uungaji wake mkono wa harakati za wanawake katika ujenzi na uendelezaji wa amani badala ya kusalia maneno matupu.  Flora Nducha na maelezo zaidi.

Sauti
3'18"