Habari Mpya

Na kwa habari za hapa na pale

Mkurugenzi mkuu wa idara ya chakula duniani WFP Bi Josette Sheeran, ameonya kwamba wakazi maskini wa mashambani barani Afrika wanakabiliwa na kimbunga kikubwa cha nyongeza za bei za chakula, mabadiliko ya hali ya hewa na muengezeko wa idadi ya watu.

Juhudi za kupunguza vifo vya watoto wadogo na mama wazazi katika mataifa yanayoendelea

UNFPA ni shirika la UM linalohusika na udhibiti bora wa idadi ya watu duniani. Mchango wa UNFPA katika kuyasaidia mataifa kuchunga afya ya jamii ni mkubwa sana, hususan katika mataifa yanayoendelea.

UNFPA yahudumia uboreshaji wa afya ya mama Tanzania

Karibuni UM ilichanganyika na Serikali za Mataifa Wanachama pamoja na mashirika ya kiraia kadhaa kuanzisha kampeni ya kimataifa, yenye lengo la kupunguza vifo vya watoto wachanga na mama wajawazito katika mataifa yanayoendelea, ikiwa miongoni mwa majukumu ya kutekeleza Malengo ya MDGs kwa wakati.

Ripoti ya UNESCO kuzingatia athari za mapigano katika ilimu

Utafiti ulioendelezwa na Shirika la UM juu ya Ilimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) kuhusu namna huduma za ilimu zinavyoathirika kutokana na mapigano imeonesha wanafunzi, walimu na vile vile wanazuoni mara nyingi hushambuliwa kihorera na makundi yanayohasimiana, kwa makusudi bila ya kisingizio.

Ban Ki-moon anasihi 'sheria za kulinda watoto ziheshimiwe'

KM Ban Ki-moon ameripotiwa akiunga mkono zile juhudi zinazoendelea za Serikali ya Chad katika kutafuta suluhu ya kuridhisha juu ya ule mgogoro wa karibuni, viliotukia nchini humo ambapo shirika lisio la kiserekali la Ufaransa, Arche de Zoé lilipojaribu kuwatorosha watoto 103 kutoka Chad bila ya idhini ya wazee wao.

Mkuu anayehudumia misaada ya kiutu kupigwa marufuku Sudan kusini

Wael al-Haj Ibrahim, mkuu wa operesheni za misaada ya kiutu Sudan amelazimishwa na Gavana wa jimbo la Darfur Kusini kuondoka kwenye eneo hilo baada ya kushtumiwa kukiuka sheria isiyobainishwa rasmi hadharani.

Afisa wa UM anasema waasi wa Darfur hawakunyimwa fursa ya kushiriki kwenye mpango wa amani

Ofisa Mkuu wa Habari katika UM, Ahmad Fawzi ambaye alihudhuria mazungumzo ya amani kwa Darfur yaliofanyika Sirte, Libya alipokutana na waandishi habari mjini New York wiki hii, baada ya kurejea mkutanoni, alisisitiza ya kwamba “fursa ya kushiriki kwenye mpango wa kurudisha amani Darfur bado ipo kwa yale makundi ya waasi wasiohudhuria kikao cha Sirte, pindi makundihayo yatakuwa tayari kujiunga kidhati na utaratibu huo.”

UM kutathminia uharibifu wa mazingira katika Ogoni, Nigeria

Shirika la UM juu ya Hifadhi ya Mazingira (UNEP) pamoja na Shirika la UM juu ya Miradi ya Maendeleo (UNDP) yamekamilisha, kwa kina, mjini Abuja, Nigeria na Serikali ya Nigeria maafikiano ya kuanzisha tathmini ya jumla kuhusu athari za mazingira zinazochochewa na shughuli za uchimbaji mafuta kwenye jimbo la Ogoni liliopo katika eneo la Nile Delta.

Alan Doss atilia mkazo ushirikiano wa kikanda kuimarisha usalama Afrika Magharibi

Mjumbe Maalumu wa KM kwa Liberia, Alan Doss katika tafrija ilioandaliwa nchini kuheshimu Watumishi wa Ulinzi wa Jumuiya ya Maendeleo ya Uchumi kwa Mataifa ya Afrika Magharibi (ECOWAS) alitilia mkazo umuhimu wa kukuza ushirikiano wao wa kikanda, juhudi ambazo anaamini ndizo zenye uwezo hakika wa kuimarisha usalama wa eneo zima la Afrika Magharibi.

UM umethibitisha marubani wa helikopta ya UNMIL ilioanguka Liberia wamefariki

UM umethibitisha kwamba ile helikopta ya kuchukua mizigo iliyoanguka karibuni kwenye mji wa Ganta, Wilaya ya Nimba, kaskazini mashariki ya Liberia ilisababisha vifo vya marubani wawili na mhandisi wa ndege kutoka Shirikisho la Urusi ambao wa kihudumia operesheni za Shirika la UM juu ya Ulinzi wa Amani Liberia (UNMIL).