Habari Mpya

Ziara ya NKM Asha-Rose Migirio Austria kuhutubia Kikao cha Kuhuisha Serekali

Naibu KM Asha-Rose Migiro Ijumanne alihutubia Kikao cha Saba cha Kimataifa kilichojumuika kwenye mji wa Vienna, Austria kuzingatia taratibu za kurudisha hali ya kuaminiana kati ya wenye madaraka wenye kuendesha serekali na raia wanaotawaliwa.

Juhudi za kimataifa kupiga vita utekaji nyara wa watoto Afrika

Majuzi wawakilishi wa mataifa zaidi ya 10 kutoka Afrika Mashariki na eneo la Maziwa Makuu walikusanyika mjini Kampala, Uganda kwenye mkutano wa Shirika la UM dhidi ya Jinai na Madawa ya Kulevya (UNODC), na walizingatia ratiba ya sheria imara dhidi ya biashara ya magendo ya kuteka nyara watu na watoto, na kuwavusha mipaka kutoka makwao na kuwapeleka kwenye maeneo mengineyo kuendeleza ajira haramu, ya lazima, inayotengua kabisa haki za kibinadamu.~~

Baraza la Usalama laarifiwa na H. Annabi ratiba ya vikosi vya mseto kwa Darfur

Wiki hii Baraza la Usalama lilikutana kwenye kikao cha faragha kusikiliza ripoti ya Hedi Annabi, Naibu Mkuu wa Idara ya UM juu ya Operesheni za Amani ambaye alielezea kuhusu ratiba ya siku zijazo inayotakikana kutekelezwa ili kuharakisha upelekaji wa kile kinachojulikana kama ‘furushi zito’ la vikosi vya mseto vya UM na AU katika Jimbo la Darfur, Sudan. Annabi alisisitiza kwenye risala yake juu ya jukumu adhimu la jumuiya ya kimataifa kuikamilisha kadhia hiyo ya amani kidharura.

UNMIS kuomboleza kifo cha mshauri wa Raisi Sudan

Shirika la UM la Kulinda Amani Sudan Kusini (UNMIS) limetangaza masikitiko yake kuhusu kifo cha Dktr Majzoub Al Khalifa, Mshauri Mkuu wa Raisi wa Sudan kilichotukia kati ya wiki.

Utekelezaji wa mafikiano na AU juu ya huduma za amani wahitajia kusawazishwa, yakiri Baraza la Usalama

Baraza la Usalama lilipata fursa ya kusikiliza ripoti juu ya matokeo ya ziara ya karibuni ya Tume yake maalumu ambayo ilitembelea Afrika, na ambayo iliongozwa shirika na Balozi Dumisani Kumalo wa Afrika Kusini pamoja na Balozi Emyr Jones-Parry wa Uingereza.

Serekali za eneo na UM zakubaliana 'ramani' ya kupambana na tatizo la njaa Pembe ya Afrika

Wajumbe wa Serekali za Djibouti, Eritrea, Ethiopia, Kenya Usomali na Uganda pamoja na wawakilishi wa UM walikutana kwa mazungumzo ya siku mbili mjini Nairobi (Kenya) wiki hii na walikubaliana kukabili kipamoja vyanzo vyenye kuchochea matatizo ya njaa katika maeneo ya Pembe ya Afrika.

Taarifa juu ya hali Usomali

Ripoti ya karibuni ya KM juu ya Usomali imeelezea maelfu ya raia bado wanaendelea kuhajiri mji mkuu wa Mogadishu katika mwezi Juni, kwa sababu ya kufumka tena mapigano.

Operesheni inayoungwa mkono na UM itawakinga watoto milioni 2 Zambia dhidi ya shurua

Kuanzia tarehe 09 hadi 14 Julai mashirika ya UM juu ya maendelo ya watoto UNICEF na afya WHO yatajumuika kuhudumia kipamoja chanjo dhidi ya shurua kwa watoto milioni 2 nchini Zambia.

UNICEF kuonya, hali ya uchumi Zimbabwe huathiri zaidi watoto

Shirika la UM juu ya Mfuko wa Maendeleo kwa Watoto (UNICEF) limeripoti kuingiwa na wasiwasi mkubwa juu ya hali ya watoto Zimbabwe. Kwa mujibu wa taarifa ya UNICEF watoto ni fungu la raia ambalo huathiriwa na kusumbuliwa zaidi na hali ya kuporomoka kwa huduma za maendeleo nchini.

MONUC kuongeza juhudi za utulivu na amani katika Jimbo la Kivu

Shirika la UM juu ya Ulinzi wa Amani katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (MONUC) karibuni limeanzisha hatua mpya za kufufua tena hali ya utulivu na amani katika jimbo la mashariki la Kivu.