Habari Mpya

Tuliangushana na sasa tutainuka pamoja kuilinda baharí

Baada ya wiki ya majadiliano na matukio mbalimbali huko Lisbon, Ureno, hatimaye mkutano wa pili wa Umoja wa Mataifa kuhusu bahari umefunga pazia leo huku wakuu wa serikali na nchi wakipitisha azimio la kisiasa kwa lengo la kuokoa bahari.

Kutambulika kimataifa Kiswahili kitaongeza wageni watakaotaka kujifunza lugha hiyo:Ali Yusuf Mwarabu

Kuelekea Siku ya Lugha ya Kiswahili duniani itakayoadhimishwa Alhamisi ya wiki ijayo Julai 7 mmoja wa wakaazi wa Chukwani Zanzibar Ali Yusuf Mwarabu anasema hatua ya lugha hiyo kutambulika kimataifa kwanza ni Fahari kubwa kwa Wazanzibari lakini pia itakuwa ni fursa nzuri kwa wageni wanaoipenda kujifunza kwa urahisi kuanzia waliko na hata kufunga safari kwenda kisiwani humo.

Wahamiaji wafariki jangwani kwa kiu:IOM

Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji IOM limesikitishwa na vifo vya wahamiaji wasiopungua 20 vilivyotokea katika jangwa la nchi ya Libya na kutoa wito  kwa mataifa ya Libya na Chad kuchukua hatua kali ili kulinda wahamiaji kwenye mpaka wa nchi hizo.

Miaka 20 ya ICC: Mambo MATANO unayopaswa kuyafahamu

Kila siku, Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) inafanya kazi kwa ajili ya haki na uwajibikaji kwa uhalifu mkubwa unaotokana na baadhi ya migogoro ya kikatili zaidi duniani. Kuhukumu uhalifu mkubwa. Kuhusisha waathirika. Kuhakikisha hukumu za haki. Kukamilisha au kusaidiana na mahakama za kitaifa. Kujenga msaada zaidi. Katika miaka yake 20 ya kwanza ya kuwepo, ICC imepata maendeleo makubwa katika dhamira yake muhimu. 

Jukumu la kusaidia wanawake wa Taliban ni letu sote: Bachelet

Umoja wa Mataifa umeusihi uongozi wa Taliban kukubali ombi la wanawake wanchi hiyo la kukaa nao na kujadiliana masuala mbalimbali ikiwemo haki zao za kibinadamu.

Sayansi na sera zishirikiane ili kusaidia bahari

Baada ya siku tano za mijadala na maonesho mbalimbali, mkutano wa pili kuhusu baharí umefikia tamati huko Lisbon nchini Ureno ambako Miguel de Serpa Soares ambaye ni Msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika masuala ya kisheria amesema mwelekeo wa kulinda na kuhifadhi baharí unatia matumaini kwa kuzingatia yaliyokubaliwa, changamoto zilizoko sambamba na fursa.  

Nchi tatu zaidi Afrika zagundua kuwa na wagonjwa wa Monkeypox

Wakati nchi tatu ambazo awali hazikuwa na historia ya kuwa na ugonjwa wa ndui ya nyani au Monkeypox zikiripoti kuwa na wagonjwa katika mataifa yao, Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ulimwenguni WHO kanda ya Afrika imetangaza kuanza kufanya kazi na mataifa ya Afrika katika kuimarisha uwezo wa nchi kufanya uchunguzi wa kimaabara ili kubaini wagonjwa hao kwa haraka na kuzuia kuenea kimya kimya kwa ugonjwa huo.

WHO yakaribisha azimio la kupunguza kwa nusu vifo na majeruhi wa ajali barabarani ifikapo 2030

Shirika la afya la Umoja wa Mataifa duniani WHO limekaribisha tamko la kisiasa au azimio litakalopitishwa na nchi wanachama wakati wa mkutano wa ngazi ya juu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kuhusu usalama barabarani duniani.  

WHO yaanzisha kituo maalum cha kusaidia wananchi wa Pembe ya Afrika

Shirika la Umoja wa Mataifa la afya ulimwenguni WHO limetangaza kuongeza shughuli zake katika ukanda wa Afrika Mashariki kwa kuanzisha kituo maalum cha huduma jijini Nairobi nchini Kenya wakati huu eneo hilo likikabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula unaosababishwa na migogoro, matukio mabaya ya mabadiliko ya tabianchi ikiwa ni pamoja na ukame mbaya zaidi kushuhudiwa katiak kipindi cha miaka 40, kupanda kwa bei ya chakula kimataifa pamoja na bei ya mafuta.

Kiwango cha kujua kusoma chaporomoka ikilinganishwa na kabla ya COVID19 :UNESCO

Shirika la Umoja wa Mataifa la elimu sayansi na utamaduni UNESCO limesema kunahitajika uhamasishaji wa pamoja ili lengo namba 4 la elimu sawa kwa wote la Malengo ya maendeleo endelevu SDGs liweze kufikiwa.