Wanawake

Uhakika wa chakula ni mtihani mkubwa kwa watu wa jamii za asili: FAO

Uhakika wa chakula umeelezwa kuwa ni changamoto kubwa kwa watu wa jamii za asili hususan wanawake ambao ndio walezi wa familia na jamii.  

Idadi ya wanawake wasionyonyesha watoto wao huko Bukoba nchini Tanzania yaongezeka- Takwimu

Wiki ya unyonyeshaji duniani ikiwa imeingia siku ya tatu, inaelezwa kuwa katika manispaa ya mkoa mmoja kaskazini-magharibi mwa Tanzania idadi ya wanawake wasionyonyesha watoto wao kwenye kipindi cha miezi sita ya mwanzo tangu kuzaliwa imeongezeka na hivyo kuhatarisha uhai wa watoto hao.

Kujifungua kwa upasuaji kwakosesha mtoto fursa ya kunyonya maziwa ya mama punde tu anapozaliwa- WHO

Umoja wa Mataifa unasema kuwa bado watoto wanakumbwa na changamoto kubwa ya kunyonya maziwa ya mama zao pale tu wanapozaliwa. Hata kwenye hospitali zenye wataalamu wabobezi bado watoto wananyimwa haki yao hiyo ambayo ni muhimu ili kuchagiza makuzi yao.

Tunapomuenzi Mandelea tuenzi kwa vitendo aliyoyakumbatia:UN

Nelson Mandelea alikuwa mtu wa vitendo na sio maneno matupu, tunapomuenzi tufanye hivyo kwa vitendo. Wito huo umetolewa hii leo kwenye na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres kwenye tukio maalumu la kumbukizi ya Mandela ambae angekuwa hai hii leo angekuwa na umri wa miaka 100 .

Uelewa wa usawa wa jinsia wabadili maisha ya kaya Ruvuma nchini Tanzania

Ainisho la suala la usawa wa kijinsia limekuwa likileta utata hasa pale ambapo jamii haijaweza kushirikishwa vyema kutambua manufaa ya suala hilo. Huko wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma nchini Tanzania,  suala hilo ambalo ni lengo namba tano la malengo ya maendeleo endelevu, SDGs sasa limeanza kushika kasi.

Maganda ya vyakula yageuzwa mkaa nchini Kenya

Ganda la muwa la jana chungu kaona kivuno! ni usemi ambao unadhihirika hivi sasa nchini  Kenya ambako shirika moja linatumia maganda ya mazao kutengeneza nishati ambayo ni mkombozi hasa kwa wanawake ambao macho yao hugeuka kuwa mekundu na kudhaniwa kuwa ni wachawi kutokana na moshi wa kuni na mkaa utokanao na miti.

Muda wa maneno umekwisha tuchukue hatua tuokoe wanawake- Bi. Mohammed

Baada ya ziara yao kwenye nchi za Sudan Kusini, Chad na Niger, viongozi wa Umoja wa Mataifa na Muungano wa Afrika pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje wa Sweden, leo wamewasilisha ripoti zao mbele ya wajumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wakati wa kikao kuhusu wanawake, amani na usalama barani humo.

Uvuvi ndio uhai wetu na maisha yetu , lakini sasa ni mtihani-Wanawake Chad

Navua samaki kwa miaka ishirini,  na sasa inazidi kuwa vigumu kupata samaki, ni kauli ya mvuvi mwanamke huko nchini Chad ambaye mabadiliko ya tabianchi na matumizi holela ya maji kwenye bonde la Ziwa Chad yameleta shida kwenye familia yake

Ziarani Chad, Naibu Katibu Mkuu apazia nafasi ya wanawake

Naibu Katibu Mkuu  wa Umoja wa Mataifa Amina J. Mohammed yuko ziarani nchini Chad ambako amesisitiza jukumu muhimu la wanawake wa nchi hiyo katika kukabiliana na changamoto za Boko Haram na uchochezi wa ukatili.

Kuna nuru Sudan Kusini licha ya changamoto- Bi. Mohammed

Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Amina J. Mohammed amehitimisha ziara yake ya siku mbili nchini Sudan Kusini hii leo akisema kuna dalili za ustawi nchini humo licha ya changamoto zilizopo.