Wanawake

WFP/Taasisi ya Mradi wa Vijiji vya Milenia zaungana kupunguza wenye njaa na utapiamlo Afrika

Kadhalika, mapema wiki hii Shirika la Miradi ya Chakula Duniani (WFP), likijumuika na mpango wa maendeleo unaoungwa mkono na UM, unaoitwa Mradi wa Vijiji vya Milenia, yameanzisha bia mradi mwengine mpya unaojulikana kama mradi wa "maeneo huru dhidi ya ukosefu wa chakula cha kutosha" utakaotekelezewa vijiji 80 katika nchi 10 za Afrika, kusini ya eneo la Sahara.

Ukame katika Uganda unaitia wasiwasi WFP

Shirika la Miradi ya Chakula Duniani (WFP) limeripoti rasmi hii leo kuingiwa wasiwasi kuhusu mfululizo wa mvua haba katika Uganda kwenye majira ya mvua, hali iliosababisha watu milioni mbili kukosa uwezo wa kupata chakula na kuomba wasaidiwe chakula na mashirika ya kimataifa kunusuru maisha.

Mashirika ya UM yamuunga mkono KM na rai ya kuanzisha idara maalumu kwa masuala ya kijinsiya

Shirika la UM juu ya Udhibiti wa Idadi ya Watu (UNIFEM) pamoja na Jumuiya Mashirika ya UM Kupambana na UKIMWI (UNAIDS) yameripoti kuunga mkono ile rai ya KM ya kufungamanisha vitengo vya UM vinavyohusika na masuala ya wanawake kuwa Idara moja.

Vifo vya watoto wachanga duniani vyaendelea kuteremka, inaripoti UNICEF

Shirika la UM juu ya Mfuko wa Maendeleo kwa Watoto (UNICEF) limetangaza takwimu mpya zilizokusanywa na wataalamu kutoka mashirika ya UM, ikijumlisha WHO, UNICEF, Benki Kuu ya Dunia na Kitengo cha UM juu Idadi ya Watu, takwimu ambazo zilionyesha viwango vya vifo vya watoto wachanga duniani, chini ya umri wa miaka mitano, viliteremka kwa asilimia 28 katika mwaka 2008.

NKM atoa mwito wa utendaji dhidi ya udhalilishaji wa wanawake

Kwenye mkutano wa mawaziri kuzingatia masuala ya udhalilishaji na matumizi ya nguvu dhidi ya wanawake, unaofanyika kwenye mji wa Roma, Utaliana, hii leo, NKM Asha-Rose Migiro aliwaambia wajumbe wa kimataifa waliohudhuria kikao hicho ya kuwa madhila ya kutumia mabavu dhidi ya wanawake yaliongezeka zaidi mnamo mwaka uliopita, kwa sababu ya kuporomoka kwa shughuli za soko la fedha la kimataifa.

UM waitaka Israel kuruhusu vifaa kuingia Ghaza haraka kufufua huduma za maji

Mratibu wa Misaada ya Kiutu kwenye Maeneo Yailokaliwa Kimabavu ya WaFalastina, Maxwell Gaylard - akijumuika na Jumuiya za Mashirika Yasio ya Kiserikali yanayoambatana na Mashirika ya Kimataifa juu ya Misaada ya Maendeleo - wametangaza leo hii taarifa maalumu yenye kuthibitisha kufanyika uharibifu mkubwa wa vifaa vya huduma za usafi na maji katika eneo la Tarafa ya Ghaza, hali ambayo inazidisha ugumu wa maisha kwa umma wa eneo hili na kuwanyima hadhi yao ya kiutu.

Mahakama ya Rufaa ya ICC imeamua aliyekuwa kiongozi wa JKK asalie kizuizini wakati akisubiri kesi

Mahakama Ndogo ya Rufaa ya Mahakama ya Kimataifa Juu ya Jinai ya Halaiki (ICC) imeamua Jean-Pierre Bemba Gombo, aliyekuwa Naibu Raisi wa JKK, aendelee kuwekwa kifungoni kabla ya kesi yake kusikilizwa na Mahakama Kuu.

Serikali zahimizwa kutekeleza ahadi za kuwasaidia wanusurika wa mabomu yaliotegwa ardhini

Ripoti mpya ya kufanikisha yenye mada isemayo "Sauti za Kutoka Ardhini" imebainisha kwamba licha ya kupatikana maendeleo katika kuangamiza akiba ya mabomu ya kutega ardhini, kutoka ghala mbalimbali, pamoja na kuziondosha silaha hizo, hata hivyo serikali za kimataifa bado zimeshindwa kutekeleza ahadi zao za kuwajumuisha waathirika wa silaha hizo kwenye maisha ya kawaida ya jamii zao.

Malaria Kenya imepunguzwa na mchanganyiko wa tiba mpya

Taarifa ya jarida linalochapishwa na Shirika la Afya Duniani (WHO) liliotolewa kwa mwezi Septemba, limebainisha ya kuwa tiba mpya iliovumbuliwa, ya mchanganyiko, ina uwezo wa kupunguza kwa kiwango kikubwa hatari ya maambukizo ya malaria kwa watoto wadogo.