Ubakaji unasalia kuwa moja ya uhalifu mbaya zaidi duniani na cha kusikitisha ni kwamba asilimia kubwa ya waathirika hushindwa kujitokeza au kushitaki uhalifu huo wakidhani kuwa ni makosa yao.
Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC mradi wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo MONUSCO wa kuelimisha jamii kuhusu ulinzi wa mtoto na ukatili wa kingono umesaidia kuongeza uelewa wa jamii kuhusu madhara ya vitendo hivyo.
Ikiwa leo ni siku ya kupinga rushwa na ufisadi duniani, Umoja wa Mataifa unataka hatua bunifu zaidi kushinda vita hivyo ambavyo vinapora rasilimali muhimu kwa ajili ya maendeleo ya wananchi. Brenda Mbaitsa na maelezo zaidi.
Muungano wa Afrika AU na shirika la chakula na kilimo la Umoja wa Mataifa FAO wamesema wanaimarisha ushirikiano wao ili kuhakikisha uchumi wa kilimo barani Afrika unaleta tija kwa mamilioni ya watu wa bara hilo.
Katika visiwa vya Pacifiki kati ya asilimia 75 hadi 90 ya wachuuzi sokoni ni wanawake na kwa kutambua umuhimu wao na mchango wao katika jamii shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya wanawake UN Women liliamua kuanzisha mradi wa masoko kwa kwa ajili ya mabadiliko au M4C kwa ajili ya kuwawezesha wanawake hao na familia zao.
Wakati dunia ikiadhimisha siku ya kimataifa kwa ajili ya kutokomeza ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na wasichana, Umoja wa Mataifa umesema umedhamiria kukomesha mifumo yote ya ukatili kwa kundi hilo kwani ni wajibu na haki kufanya hivyo.
Mkataba wa kimataifa wa haki za mtoto CRC ambao mwaka huu umetimiza miaka 30 tangu upitishwe na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, unataja bayana haki kuu nne za msingi ambazo kile mtoto, yaani mkazi wa dunia mwenye umri wa miaka 18 au chini ya hapo anapaswa kuzipata awe wa kike au wa kiume.
Pamoja na kukabiliwa na ubaguzi na unyanyasaji wa kingono, wanawake nchini Jamhuri ya Afrika ya kati, CAR, wamechukua hatua ya kuwapatia matumaini wenzao wanaorejea katika makazi yao walimofurushwa kutoka na mapigano katika jamii zao.