Wanawake

Uandikishaji kura ya maoni Kaskazini mwa Sudan hauridhishi:UM

Kumekuwa na mwamko mgodo wa wananchi wa Sudan Kusin ambao wanaishi upande wa pili yaani Sudan Kaskani wanaojitokeza kujiandikisha kwenye daftari la upigaji kura kwa ajili ya kura ya maoni itayofanyika January mwakani.

Mipango miji salama kwa wanawake yazinduliwa Delhi

Shirika la Umoja wa Mataifa la maendeleo ya akina mama limezindua mpango wa kimataifa wa kuifanya miji kuwa salama kwa wanawake mjini New Delhi nchini India wakati wa kuanza kwa mkutano wa kimataifa kuhusu usalama wa wanawake.

IOM yaunga mkono matembezi ya kupinga dhuluma za kijinsia

Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM kwa ushirikiano na wizara ya masuala ya uchumi na jamii nchini Equador litatoa mchango kwa serikali za mitaa mashirika ya kitaifa na kimataifa na yasiyokuwa ya umma kwenye matambezi juma hili ya kupinga dhuluma za jinsia.

Haki za binadamu nchini Iran zinatia mashaka:Navi Pillay

Kamishina mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Navi Pillay leo Jumanne amerejea kuelezea hofu yake juu ya hatma ya watetezi wa haki za binadamu nchini Iran na hasa Bi Nasrin Sotoedeh ambaye amekuwa kwenye mgomo wa kula kwa wiki kadhaa kwenye gereza la Evin mjini Tehran.

Uwekezaji katika sekta ya kilimo lazima ukuwe:FAO

Mkurugenzi mkuu wa shirika la chakula na kilimo duniani FAO Jacques Diouf leo amesema hakikisho la kukabili matatizo ya muda mrefu ya chakula duniani ni kuwekeza katika kilimo.

Waathirika wa mafuriko Pakistan wahofia majira ya baridi:ICRC

Maelfu ya waathirika wa mafuriko ya Pakistan kwenye jimbo la Khyber Pakhtunhkwa wanakimbizana na wakati kabla ya kuwasili kwa majira ya baridi, hasa kujenga upya nyumba zao, kuondoa mabaki ya uharibifu wa mafuriko na kupanda mazao.

Wafanyakazi wa mashambani ndio waathirika wa HIV:IOM

Ripoti mpya ya shirika la kimataifa la uhamiaji IOM inasema maambukizi ya virusi vya HIV ni ya juu miongoni mwa wafanyakazi wa mashambani nchini Afrika ya Kusini.

Kipindupindu bado ni changamoto kubwa Haiti:WHO

Vifo vilivyosababishwa na kipindupindu nchi Haiti vimeongezeka na kufikia 1300 huku wengine zaidi ya 23,000 wameathirika kwa mujibu wa shirika la afya duniani WHO.

Mashoga kupata msukomo kupambana na HIV:UNAIDS/WHO

Mpango wa Umoja wa Mataifa wa kupambana na ukimwi UNAIDS na shirika la afya duniani WHO wamekaribisha matokeo ya utafiti yaliyochapishwa leo yanayoonyesha kwamba kuna njia ya kuweza kusaidia kukinga maambukizi miongoni mwa wanaume wanaofanya mapenzi ya njinsia moja.

Maambukizi mapya ya virusi vya HIV na ukimwi yanapungua duniani:UNAIDS

Idadi ya watu wapya wanaoambukizwa virusi vya HIV na ukimwi inapungua kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na mpango wa pamoja kupambana na ukimwi wa Umoja wa Mataifa UNAIDS.