Mwakilishi maalumu wa mpango wa kulinda amani Darfur wa Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika UNAMID Ibrahim Gambari leo amelieleza baraza la usalama kuhusu hali ya jimbo hilo la Sudan.
Wadau wa misaada nchini Kyrgyzstan leo wametoa wito mpya wa dola milioni 96 kwa ajili ya kuwasaidia eneo la kusini mwa nchi hiyo kulikozuka machafuko mwezi Juni na kuathiri watu 400,000.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon leo ametoa wito wa juhudi zaidi za kimataifa za ajenda ya kutokomeza silaha za nyukilia, akisisitiza kwamba kufanya hivyo ni njia pekee ya kuhakikisha usalama kwa wote.
Mkutano wa 15 wa viongozi wa nchi za umoja wa Afrika AU uliomalizika leo mjini Kampala Uganda umeafikiana kuongeza majeshi zaidi ya kulinda amani nchini Somalia.
Ripoti mpya ya shirika la maendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP inasema watu katika nchi za Amerika ya Kusini na visiwa vya Carebeani ndio walio na tofauti kubwa kabisa duniani ya utajiri na kipato.
Kuongeza idadi ya wanawake wa Iraq katika utatuzi wa migogoro na kutafuta amani ya kudumu ni miongoni mwa mada zilizojadiliwa leo mjini Baghdad katika kongamano lililoandaliwa na Umoja wa Mataifa.