Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa limefiakia maafikiano yasiyo rasmi ya kuanzisha chombo maalumu kimoja cha kuchagiza usawa kwa wanawake. Katika hatua ya kihistoria leo baraza kuu la Umoja wa Mataifa limepiga kura ya bila kupingwa kuanzisha chombo hicho ili kuvuta kasi ya mchakato wa kuyafanyia kazi mahitaji ya wanawake na wasichana kote duniani.
Pamoja na kuzitaka pande zinazopigana kuheshimu maeneo ya Hospitali, mashambulizi yame endelea kwa siku ya tatu sasa karibu na Hospitali ya Keysaney Mashariki mwa Mogadishu nchini Somalia.
Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhumia Wakimbizi la UNHCR limepanda zaidi ya miti milioni 19 katika mpango maalum wa upandaji miti Kaskazini Mashariki wa Khartoum nchini Sudan.
Baraza la jamii na uchumi ECOSOC limehitimisha majadiliano yake ya siku mbili ya ushirikiano wa maendeleo kwa wito wa haja ya haraka ya kuwa na mipango ya kufikia malengo ya maendeleo ya milenia hapo 2015.
Mpango mpya wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo MUNUSCO leo tarehe mosi Julai ndio unaanza kazi rasmi kuchumua nafasi ya MONUC.
Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu UNFPA Thoraya Ahmet Obaid amesema utamaduni ni kuhusu kuhodhi mabadiliko na hakuna mabadiliko yatakayokuja kutoka nje.