Shirika la chakula duniani FAO limewatolea wito wahisani wa kimataifa kuunga mkono mpango wa uwekezaji wa dola milioni 700 katika sekta ya kilimo ya Haiti.
Kitengo cha Umoja wa Mataifa cha msaada wa kutafuta amani kimeamua kushirikiana na mashirika mengine ya Umoja wa Mataifa ,ili kuzuia ukatili wa kimapenzi katika maeneo ya migogoro na kutoa msaada unaohitajika kwa waathirika.
Mshauri wa masuala ya kuwalinda watoto wa kamati ya kimataifa ya msalaba mwekundu ICRC Kristin Barstad amesema , tetemeko la ardhi lililoikumba Haiti hivi karibuni limewaathiri vibaya watoto hasa waliopoteza wazazi wao.
Umoja wa Maita umewaalika waandishi wa habari, wawakilishi wa mashirika yasiyo ya kiserikali, wanafunzi na wanazuoni kushiriki mjadala unaofanyika kwenye mtandao kuhusu "Wanawake na vyombo vya habari."
Hatua ya hivi karibuni ya kuendelea kuwaachilia askari watoto wanaoshiriki vita kaskazini magharibi mwa Chad ,inafanya idadi ya watoto wanaorejeshwa katika maisha ya kawaida tangu mwaka 2009 kufikia 240.
Shirika la mpango wa chakula duniani WFP limekuwa likitoa msaada wa dharura wa chakula kwa watu takribani lakini tatu katika maeneo mbalimbali ya Sudan Kusini.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon, mwishoni mwa juma ametoa wito wa kuungwa mkono na viongozi wa Afrika katika kampeni yake ya kumaliza ukatili dhidi ya wanawake uliomea mizizi katika bara hilo. Ambao amesema ni kikwazo kikubwa cha maendeleo barani humo.
Wamishonari 10 kutoka kundi la Marekani lijulikanalo kama New Life Refuge walikamatwa kwenye mpaka Santo Domingo wakiwa na watoto 33 wa Kihatiti bila ya kuwa na vibali vya aina yoyote vya kuwachukua watoto hao, na wala ushahidi kuwa watoto hao ni yatima.