Wanawake

Ripoti ya UNFPA inasisitiza umuhimu wa wanawake katika kupiga vita mabadiliko ya hali ya hewa

Shirika la UM juu ya Udhibiti wa Idadi ya Watu (UNFPA) limeripoti Ijumatano kwamba, kwa kulingana na fafanuzi za taasisi yao, fungu kubwa la jamii ya kimataifa yenye kusumbuliwa, kwa uzito mkubwa kabisa na matatizo yanayoletwa na mabadiliko ya hali ya hewa, huwa ni wanawake.

UM yahimiza Mataifa Wanachama yote kushirikiana kufyeka njaa duniani

Josette Sheeran, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Miradi ya Chakula Duniani (WFP), kwenye risala aliotoa mnamo siku ya pili ya Mkutano Mkuu wa Dunia juu ya Udhibiti Bora wa Akiba ya Chakula unaofanyika Roma, Utaliana, alisema raia wote wa kimataifa - na sio viongozi wa dunia pekee - wanawajibika kuhamasishwa wajitayarishe kuwapatia chakula watu bilioni moja ziada wenye kusumbuliwa na tatizo la njaa sugu ulimwenguni.

Siku ya Kudhibiti Kisukari Duniani

Ijumamosi, tarehe 14 Novemba, iliadhimishwa kuwa ni Siku ya Kudhibiti Maradhi ya Kisukari Duniani.

Viongozi wa kimataifa wameakhirisha jukumu la kukamilisha itifaki ya Copenhagen juu ya mabadiliko ya hali ya hewa

Imeripotiwa hii leo kwamba viongozi wa kimataifa wameafikiana kuakhirisha yale majadiliano ya kufikia mapatano juu ya mabadiliko ya hali ya hewa katika mkutano ujao utakaofanyika mwezi Disemba katika Copenhagen, na badala yake wamekubaliana kwamba mkutano huu wa mabadiliko ya hali ya hewa ujaribu kufikia itifaki isio na uzito "wenye masharti ya kisiasa" ili kuwawezesha wajumbe wa kimataifa kuhakikisha masuala magumu yenye kutatanisha majadiliano yao yatazingatiwa kidhati katika siku za baadaye.

Viongozi wa dunia wakutana Roma kuzingatia mradi wa kupiga vita njaa

Mkutanao mkuu wa UM, wa siku tatu unaozingataia udhibiti bora wa akiba ya chaklula duniani, umefunguliwa rasmi leo hii kwenye mji wa Roma, Utaliana ambapo KM Ban Ki-moon, kwenye risala yale alionya kwa kukumbusha mnamo siku ya leo pekee watoto 17,000 watafariki duniani kwa sababu ya kusumbuliwa na njaa - ikijumlisha kifo cha mtoto mmoja katika kila nukta tano za dakika - jumla ambayo kwa mwaka inakadiriwa kukiuka vifo milioni 6 vya watoto, licha ya kuwa sayari yetu imebarikiwa chakula cha kuweza kutosheleza mahitaji ya chakula kwa umma wote wa kimataifa, alisisitiza KM.

Hatua ziada zinahitajika Sudan Kusini kudhibiti uhaba wa chakula, anasema Ofisa wa UM

Hilde F. Johnson, Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la UM juu ya Mfuko wa Maendeleo kwa Watoto (UNICEF) ametoa mwito unaopendekeza kuchukuliwe hatua ziada Sudan Kusini, ili kudhibiti tatizo la upungufu mkubwa wa chakula, uliojiri kwa sasa, katika baadhi ya sehemu za eneo, ili hali isije ikageuka kuwa janga baya zaidi.

UNICEF inasema watoto wanavia kwa sababu ya upungufu sugu wa chakula

Shirika la UM juu ya Mfuko wa Maendeleo kwa Watoto (UNICEF) nayo pia imewasilisha ripoti maalumu inaozingatia athari za ukosefu wa chakula kwa watoto wachanga.

Lengo la MDGs kupambana na UKIMWI linafanyiwa mapitio na UNAIDS

Jumuiya ya Mashirika ya UM dhidi ya UKIMWI (UNAIDS), kwenye makala iliochapishwa wiki hii katika Jarida juu ya UKIMWI, imezingatia kwa makini zaidi, suala la kama jamii ya kimataifa itafanikiwa kuzuia maambukizi ya UKIMWI katika 2015, kwa kulingana na pendekezo rakamu ya sita ya Malengo ya Maendeleo ya Milenia (MDGs).

OCHA inasihi, misaada ya dharura yahitajika kuunusuru umma wa Usomali na majanga ya kiutu

Ofisi ya UM juu ya Misaada ya Dharura (OCHA) imeihimiza jumuiya ya kimataifa, kuharakisha michango ya dharura inayotakikana kunusuru maisha kwa raia wa Usomali.

Nchi maskini 31 zimedhurika na bei ya juu ya chakula: FAO

Shirika la UM juu ya Chakula na Kilimo (FAO) limehadharisha kwamba ulimwengu unakabiliwa na uhaba mkubwa, na wa hatari wa chakula, ulioathiri vibaya sana nchi 31.