Wanawake

Hali ya kijamii kwa watoto na wanawake Zimbabwe ni mbaya, inasema UM

Shirika la UM juu ya Mfuko wa Maendeleo kwa Watoto (UNICEF) likijumuika na Serikali ya Zimbabwe leo limetangaza takwimu mpya za maendeleo ya jamii, takwimu zenye kuonyesha hali ya wanawake na watoto wadogo katika Zimbabwe inaendelea kuharibika na kuwa mbaya zaidi.

Mtandao mpya wa kuwasaidia Viongozi Wanaume dhidi ya Udhalilishaji wa Kijinsia, waanzishwa rasmi na KM

Asubuhi ya leo, KM ameanzisha Mtandao wa Viongozi Wanaume wa kukomesha vitendo vya kutumia mabavu na vurugu dhidi ya wanawake, Mtandao utakaojumlisha wanaume vijana pamoja na wale wenye umri mkubwa, washiriki ambao waliahidi kufyeka karaha ya kutumia nguvu ya udhalilishaji wa kijinsia.

UNICEF itaandaa warsha maalumu Copenhagen, kwa watoto kuzingatia mageuzi ya hali ya hewa

Warsha Maalumu wa Watoto Kuzingatia Masuala juu ya Mabadiliko ya Hali ya Hewa Duniani unaandaliwa kufanyika kwenye mji wa Copenhagen kuanzia Novemba 28 mpaka Disemba 04 (2009), kabla ya Mkutano Mkuu wa UM juu ya Udhibiti wa Athari za Mabadiliko ya Hali ya Hewa kuanza majadiliano.

Hali ya wasiwasi katika Equateur (JKK) imefumsha mapigano ya kikabila: OCHA

Ofisi ya UM juu ya Misaada ya Dharura (OCHA) imeeleza kuzuka kwa hali ya wasiwasi hivi karibuni, kwenye Jimbo la Kaskazini la Equateur, katika JKK, baina ya jamii za makabila ya Boba na Lobala. Hali hii inaripotiwa iliripusha mapigano makali ya kikabila mnamo tarehe 04 Novemba (2009) ambapo watu 37 walisemekana waliuawa, jumla ambayo UM inaamini ilikaribia watu 100 waliouliwa kwa sababu ya uhasama.

Tume ya WHO yazuru Usomali kutathminia hali ya afya nchini

Mnamo mwisho wa wiki iliopita, ujumbe maalumu wa hadhi ya juu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) ulizuru Usomali kutathminia hali mbaya ya afya ilioselelea nchini humo.

Maambukizo mapya ya VVU yateremka kwa 17% duniani - maendeleo zaidi yashuhudiwa kusini ya Sahara

Ripoti iliotolewa wiki hii bia na Jumuiya ya Mashirika ya UM dhidi ya UKIMWI (UNAIDS) pamoja na Shirika la Afya Duniani (WHO), imethibitisha kwamba ile miradi kinga dhidi ya maambukizo ya virusi vya UKIMWI ndio mipango ilioyawezesha mataifa kuleta tofauti halisi kwenye udhibiti unaoridhisha wa maradhi kwenye maeneo yao.

Mtetezi wa haki za watoto asema kasumbuliwa sana na ripoti za watoto wanaoshirikishwa na wapambanaji katika Sudan

Radhika Coomaraswamy, Mjumbe Maalumu wa KM juu ya Haki za Watoto Walionaswa kwenye Mapigano, ameripotiwa kuwa ana wasiwasi juu ya taarifa alizopokea, zinazoonyesha watoto walio chini ya umri wa utu uzima, wameruhusiwa kujiunga na makundi ya waasi wa katika Sudan.

Fafanuzi fupi juu ya mkutano wa UNIFEM kwa wanawake wa Darfur Kaskazini

Mnamo wiki iliopita, wanawake 500 ziada, kutoka fani na kazi mbalimbali walikusanyika katika Chuo Kikuu cha El Fasher, Darfur Kaskazini kusailia amani na utulivu kwenye eneo lao, na taifa, kwa ujumla.

Ripoti ya Hali ya Watoto Duniani 2009 - UNICEF

Shirika la UM juu ya Mfuko wa Maendeleo kwa Watoto (UNICEF) limewasilisha ripoti muhimu Alkhamisi inayosailia: Hali ya Watoto Duniani.

UNICEF inaunga mkono utekelezaji wa Mkataba wa Haki ya Mtoto kimataifa

Philip O\'Brien, Mkurugenzi wa Shirika la UM juu ya Mfuko wa Maendeleo kwa Watoto (UNICEF) anayehusika na Uchangishaji Pesa na Mashirkiano aliwaambia waandishi habari Geneva Alkhamisi ya leo,