Wanawake

Huduma za kugawa chakula Ghaza zimesimamishwa, kwa muida, na UM

KM ameshtumu mashambulio ya vikosi vya Israel dhidi ya misafara ya malori ya UM, yaliokuwa yamechukua misaada ya kiutu kwa wakazi wa eneo la Ghaza, ambapo wafanyakazi wawili wa UNRWA waliuawa, licha ya kuwa wenye madaraka wamepatiwa taarifa kamili kuhusu misafara hiyo.

UNHCR yaihadharisha BU juu ya matatizo ya kuhifadhi wahamiaji duniani

Antonio Guterres, Kamishna Mkuu wa Shirika la UM juu ya Huduma za Wahamiaji (UNHCR) asubuhi ya leo amehutubia Baraza la Usalama kuhusu vizingiti vinavyokabili shirika katika kuhudumia makumi milioni ya wahamiaji waliong’olewa makwao katika sehemu mbalimbali za dunia, kutokana na hali ya mkorogano na hatari iliopamba sasa hivi kwenye mazingira ya kimaaifa.

Mashambulio ya Israel yaua darzeni za watu kwenye skuli za UM Ghaza

Hii leo, vurugu la eneo liliokaliwa la WaFalastina, katika Tarafa ya Ghaza, limeingia siku ya 11 tangu vikosi vya Israel vilipoanzisha operesheni za kijeshi pamoja na mashambulio kwenye eneo hilo.

UNRWA yahadharisha 'hali mbaya ya Ghaza lazima idhibitiwe haraka kunusuru maisha ya umma'

Shirika la UNRWA linasema kuna dharura ya kusimamisha mapigano na vurugu katika Ghaza, haraka iwezekanavyo, ili kuhakikisha kunapatikana angalau upenu utakaoruhusu misaada ya kiutu, ya dharura, kuingizwa kwenye eneo la mtafaruku na kunusuru maisha ya umma waathirika, umma ambao sasa hivi hauana mahali pengine salama pa kukimbilia.

Suluhu ya mzozo wa Ghaza ipo na UM, asisitiza KM

Imetangazwa asubuhi ya leo kwamba KM Ban Ki-moon atakutana, Ijumanne, na mawaziri wa nchi za kigeni wa kutoka mataifa ya KiArabu, pamoja na wadau wengine muhimu, ili kutathminia taratibu za pamoja za kuhamasisha Baraza la Usalama kuchukua hatua za haraka ili kusitisha mapigano katika Ghaza, na kuiwezesha jumuiya ya kimataifa kuhudumia vizuri zaidi misaada ya kiutu, kwa

50,000 wang'olewa makazi Usomali kufuatia uhasama

Kuhusu habari nyengine, Mark Bowden, Mratibu Mkazi wa Misaada ya Kiutu katika Usomali, alibainisha wasiwasi mkuu kuhusu hali katika jimbo la Galgaduud, Usomali ya kati, baada ya kuzuka, wiki iliopita, mapigano mapya ambapo watu 40 ziada waliuawa na zaidi ya watu 50,000 walilazimika kung’olewa makwao na kuelekea kwenye maeneo mengine kutafuta usalama.