Wanawake

Twamkumbuka Mama Afrika - Miriam Makeba

Tarehe 27 Novemba 2008 ni Siku Kuu ya Kutoa Shukrani nchini Marekani, na kawaida ofisi zote hufungwa, ikijumuisha vile vile ofisi za Makao Makuu ya UM, ziliopo jiji la New York, Marekani. Hata hivyo, Idhaa ya Kiswahili ya Redio ya UM imewajibika kutayarisha vipindi katika siku hii. Ilivyokuwa hii ni Siku Kuu ya Kutoa Shukrani, nasi pia tumeamua kuandaa makala maalumu, yenye kuwasilisha shukrani za jumuiya ya kimataifa, kwa ujumla, kuhusu mchango wa Balozi Mfadhili wa Shirika la UM juu ya Chakula na Kilimo (FAO), Mama wa Afrika, msanii maarufu wa Afrika Kusini, marehemu Miriam Makeba katika kuhudumia kihali umma uliokabiliwa na matatizo ya ufukara na hali duni.~

Mkutano Mkuu III kukomesha madhila ya kijinsia dhidi ya watoto na vijana waendelea Rio de Janeiro

Mkutano Mkuu wa Tatu Dhidi ya Ukandamizaji wa Kijinsia wa Watoto na Vijana, unaofanyika Rio de Janeiro, Brazil umeingia siku ya pili na utaendelea na mijadala yake hadi Ijumaa, tarehe 28 Novemba. Mkutano huu umeandaliwa bia na Serikali ya Brazil, mamshirika ya kiraia na Shirika la UM juu ya Mfuko wa Maendeleo kwa Watoto (UNICEF).

UNICEF inahimiza juhudi za kimataifa zikithirishwe kuhudumia maisha bora watoto wa Afrika

Ripoti ya mwaka ya Shirika la UM juu ya Mfuko wa Maendeleo kwa Watoto (UNICEF) kuhusu “Hali ya Watoto wa Afrika katika 2008” imeeleza kwamba eneo hilo, hasa lile liliopo kusini ya Sahara, ni mwahala pagumu kwa mtoto kuendeleza maisha.

UM unaadhimisha Siku ya Kimataifa Kukomesha Udhalilishaji wa Kijinsiya

UM na mashirika yake kadhaa ulimwenguni yanaiadhimisha siku ya leo kuwa ni Siku ya Kimataifa ya Kukomesha Utumiaji Nguvu dhidi ya Wanawake.

Mataifa Wanachama 125 yanakutana Rio kusailia hifadhi ya watoto na vijana dhidi ya ukandamizaaji wa kijinsiya

Wajumbe karibu 3,000 kutoka nchi 125, wamekusanyika hii leo kwenye mji wa Rio de Janeiro, Brazil kuhudhuria kikao cha siku nne cha Mkutano Mkuu wa Tatu kukomesha dhidi ya Ukandamizaji wa Kijinsiya dhidi ya Watoto na Vijana Ulimwenguni.

Mapigano yawanyima wanafunzi 150,000 fursa ya kuilimishwa katika JKK: UNICEF

Veronique Taveau, Msemaji wa Shirika la UM juu ya Mfuko wa Maendeleo kwa Watoto (UNICEF) aliwaambia waandishi habari wa kimataifa Geneva, ya kwamba kutokana na mapigano yaliotanda katika JKK, skuli kadha zimelazimika kufungwa katika eneo la Rutshuru, na ambayo wanafunzi 150,000 ziada wananyimwa fursa ya masomo, maana hali ni ya wahka mkubwa na ya hatari sana.

Charlize Theron aidhinishwa rasmi kuwa Mjumbe wa Amani dhidi ya Unyanyasaji wa Wanawake

Mwigizaji wa kike wa michezo ya sinema kutoka Afrika Kusini na Marekani, Charlize Theron leo ameidhinishwa rasmi na kukabidhiwa wadhifa wa Mjumbe Maalumu wa UM kwa Amani, na anatumainiwa kuchangisha huduma zake kwenye juhudi za kukomesha udhalilishaji na utumiaji mabavu dhidi ya wanawake, hususan katika bara la Afrika.~

UNICEF ina wahka na usalama wa watoto katika eneo la mashariki la JKK

Shirika la UNICEF limeripoti kukithirisha huduma za kugawa maji safi ya kunywa pamoja na vifaa vya kusafishia maji katika sehemu za JKK, kwa lengo la kuhakikisha umma muathiriwa unapatiwa kinga ziada dhidi ya hatari ya kufumka kipindupindu.