Wanawake

UNICEF inasema kunyonyesha watoto kunafaidisha afya

Shirika la UM juu ya Mfuko wa Maendeleo kwa Watoto (UNICEF) likijumuika na Shirika la Afya Duniani (WHO) na pia Umoja wa WABA ambao huendeleza miradi ya kimataifa ya unyonyeshaji, wametoa mwito wa pamoja unaopendekeza kuongezwe misaada ya miradi ya kuwahimiza akina mama wazazi wa kimataifa kunyonyesha watoto wao ili kuwakinga watoto wachanga na maambukizo ya magonjwa hatari na maututi ya kitoto.

Mawaziri wa Maziwa Makuu wamekusanyika Kinshasa kuzingatia taasisi ya haki za wanawake

Mawaziri wanaohusika na haki za wanawake kutoka mataifa 11 ya Maziwa Makuu katika Afrika wameanza, Alkhamisi (24/07/08) mijadala ya siku mbili kwenye mji wa Kinshasa, katika Jamhuti ta Kideomkrasi ya Kongo (JKK) kuzingatia hatua za kuchukuliwa kipamoja kuanzisha taasisi mpya ya kikanda itakayoendeleza utafiti juu ya haki za kijinsiya na kushughulikia huduma za kuhifadhi nyaraka zinazoambatana na kadhia hiyo.

Siku ya Kudhibiti Idadi ya Watu Duniani

Tarehe 11 Julai huadhimishwa kila mwaka na UM kuwa ni Siku ya Kudhibiti Idadi ya Watu Duniani. Risala ya KM Ban Ki-moon pamoja na Thoraya Ahmed Obaid, Mkurugenzi wa Shirika la UM juu ya Mfuko wa Kudhibiti Mifumko yaIdadi ya Watu (UNFPA) kuadhimisha siku hiyo imekumbusha tena kwamba lengo la 5 la MDGs la kupunguza vifo vya uzazi limezorota duniani na lipo nyuma ya maendeleo yote mengine ya milenia na linahitajia kurekibishwa haraka ili uzazi wa majira udhibitiwe vyema na kunusuru maisha ya mama na watoto kwenye nchi masikini. ~ ~~

Kikao cha CEDAW chazingatia haki za wanawake Tanzania

Wawakilishi kadha wa kimataifa walikusanyika kwenye Makao Makuu ya UM kuanzia tarehe 30 Juni kuhudhuria kikao cha mwaka cha Kamati ya Kuondosha Ubaguzi Dhidi ya Wanawake (CEDAW), kwa madhumuni ya kufanya mapitio juu ya namna Mataifa Wanachama yalioridhia Mkataba wa CEDAW yanavyowatekelezea wanawake haki zao. Miongoni mwa Mataifa manane yaliowakilisha ripoti za mapitio mbele ya Kamati mwaka huu, kwenye kikao cha 41, ilijumuisha pia Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

UNHCR inafuatilia kwa makini sera ya EU juu ya haki za wahamiaji

Shirika la UM juu ya Huduma za Wahamiaji (UNHCR) limetangaza kuwa linafuatilia kwa uangalizi mkubwa kabisa majadiliano ya wanachama wa Umoja wa Ulaya (EU) kuhusu mswada wa Maafikiano ya Ulaya juu ya Hifadhi ya Kisiasa na Wahamiaji. Jennifer Pagonis, Msemaji wa UNHCR, alitupatia dokezo kuhusu mswada huo alipozungumza na waandishi habari Ijumanne mjini Geneva.~~