Wanawake

Maradhi ya IDD yanahitajia msukumo ziada kunusuru akili watoto: UNICEF

Ripoti ya Shirika la UM juu ya Mfuko wa Maendeleo kwa Watoto (UNICEF) kuhusu maradhi ya ukosefu wa iodine au maradhi ya IDD, imeeleza kupatikana mafanikio makubwa ulimwenguni kwenye huduma za afya za kukabiliana na ugonjwa huo kutokana na michango ya Serikali, jamii na viwanda vya chumvi.

Udhalilishaji wa kijinsiya unazingatiwa na Baraza la Usalama

Baraza la Usalama chini ya uraisi wa Marekani kwa mwezi Juni, Alkhamisi linasailia na kujadilia suala la kukomesha vitendo karaha vya kunajisi wanawake kimabavu, kwenye mazingira ya uhasama na mapigano. Mwenyekiti wa kikao hiki cha hadhi ya juu ni Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Condoleezza Rice.

Nambari maalumu ya simu yapendekezwa na ITU kuhifadhi watoto duniani

Shirika la Kimataifa la Mawasiliano ya Simu (ITU) leo mjini Geneva, limetoa mwito uzitakayo Nchi Wanachama zote kuanza kutumia nambari maalumu ya simu, kwa makusudio ya kuhudumia watoto wanaohitajia misaada ya dharura, ya kihali au kijamii.

Mradi wa Milenia, Mbola watathminiwa na Mtafiti Mwandamizi

Katika makala zilizopita tulijadilia juhudi za za kuondosha umasikini za wanakijiji wa Mbola, na pia kuelezea ushirikiano walionao na wataalamu wa kitaifa, na kimataifa, kwa makusudio ya kuwasilisha mafanikio ya muda mrefu kwenye eneo lao, mafanikio ambayo yatafaidisha umma, kijumla.~~

Usawa wa Kijinsiya Makazini unasisitizwa na ILO

Shirika la UM juu ya Haki za Wafanyakazi Duniani (ILO) limeanzisha kampeni mpya ya kimataifa itakayoendelezwa kwa muda wa mwaka mmoja, iliokusudiwa kuangaza umuhimu wa kuwa na usawa wa kijinsia katika mifumo ya kazi na ajira. Kadhia hii inalingana na mapendekezo ya Ajenda ya Kazi Stahifu, ambayo inajumuisha mada 12 zinazotumiwa kupitia athari za mifumo ya kazi na ajira miongoni mwa wafanyakazi wanaume na wanawake, na kufafanua kama haki zao hutekelezwa kwa usawa. ~~

Wakati umewadia kukomesha kwa vitendo utumiaji mabavu dhidi ya Wanawake

Wiki hii Naibu KM Asha-Rose Migiro alipata fursa ya kuzungumzia suala la udhalilishaji wa kijinsia, kwenye mkutano maalumu uliotayarishwa mjini New York na Halmashauri ya Mataifa ya Ulaya pamoja na Ubalozi wa San Marino katika UM. Kwenye risala alioitoa mbele ya kikao hicho NKM Migiro alihimiza kuchukuliwe hatua za pamoja, kukomesha haraka tabia ya utumiaji nguvu na mabavu dhidi ya wanawake, hatua ambayo ikikamilishwa, alitilia mkazo, itawavua wanawake na mateso hayo maututi.~

Ripoti juu ya juhudi za kufufua nafasi za elimu mitaani Kenya

Wiki hii tuna ripoti kuhusu juhudi za kufufua huduma za elimu ya msingi katika Kenya, ambazo ziliharibiwa na machafuko yaliotukia nchini humo kufuatia uchaguzi wa mwisho wa 2007.~

Baraza la Haki za Binadamu linazingatia haki za wanawake

Louise Arbour, Kamishna Mkuu wa UM juu ya Haki za Binadamu aliwaambia wajumbe waliohudhuria majadiliano ya Baraza la Haki za Binadamu (HRC) mjini Geneva, kuzingatia haki za wanawake kwamba bila ya kuwepo sheria za kuwakinga wanawake na mateso, pamoja na utumiaji mabavu dhidi yao, serikali za kimataifa na wote waliodhaminiwa madaraka ya utawala hawatofanikiwa kutekeleza usawa wa kijinsia kuimarisha maendeleo yao:~~