Wanawake

Fafanuzi za Mjumbe wa Afrika Mashariki kuhusu kikao cha mwaka cha CSW

Kamisheni ya UM juu ya Haki ya Wanawake Duniani (CSW)ilikusanyisha wajumbe kadha wa kadha wa kimataifa, kwenye Makao Makuu ya UM, waliohudhuria kikao cha mwaka, cha 52, ambapo kuanzia tarehe 25 Februari hadi Machi 07, 2008 wajumbe hawa walizingatia kipamoja yale masuala yanayohusu haki za wanawake.

'Ufunguo wa kuyafikia Malengo ya Milenia umo mikononi mwa wanawake', anasihi NKM

Mapema wiki hii, Naibu KM wa UM, Asha-Rose Migiro aliwahutubia wanachama wa Baraza la Marekani juu ya Uhusiano wa Kimataifa (Council on Foreign Relations) liliopo mjini New York, ambapo alisailia mada iliotilia mkazo kaulimbio isemayo ‘wanawake ndio wenye ufunguo wa kuyafikia Malengo ya Maendeleo ya Milenia (MDGs)kwa wakati na kupunguza umasikini na hali duni kwa nusu, itakapofika 2015.”

UM inaadhimisha Sikukuu ya Wanawake wa Kimataifa kwa 2008

UM huadhimisha tarehe 8 Machi kila mwaka kuwa ni Siku ya Wanawake wa Kimataifa. Ilivyokuwa tarehe hiyo mwaka huu imeangukia Ijuammosi, taadhima za kuisherehekea Siku hiyo zilifanyika Makao Makuu Alkhamisi ya tarehe 06 Machi kabla ya mwisho wa wiki kuwasili.

Watoto waliotoroshwa Chad kurejeswha kwa aila zao

Watoto 100 ziada, wingi wao wakiwa raia wa Chad, ambao miezi mitano iliopita walitaka kutoroshwa na kupelekwa nje na shirika wahisani la Kifaransa la Zoe’s Ark, wanatazamiwa kurejeshwa kwa wazee wao mnamo siku za karibuni.