Wanawake

Nishati ya sola yaongeza kasi ya ajira duniani

Kama bado unapuuza suala la nishati jadidifu ikiwemo ile ya sola, ni wakati wa kuchukua hatua sasa kwani ripoti mpya iliyotolewa leo na shirika la kimataifa la nishati jadidifu, IRENA na lile la Umoja wa Mataifa la kazi duniani, ILO imethibitisha ukuaji wa ajira kwenye sekta ya nishati jadidifu na kutaka mikakati ya kuweka mnyonyoro tulivu wa thamani na ajira zenye hadhi, ikisema mwaka jana idadi ya ajira kwenye sekta hiyo ilifikia milioni 12.7, ikiwa ni ongezeko la ajira mpya 700,000 licha ya janga la COVID-19.

Wanawake viongozi ni chachu ya mabadiliko chanya kwenye jamii

Hii leo kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa kandoni mwa mjadala mkuu wa Baraza Kuu, Wanawake wakuu viongozi wa nchi na serikali wamezungumzia nafasi muhimu ya uongozi wa wanawake kwenye kutatua changamoto zinazokabili dunia hivi sasa sambamba na kujenga mustakabali endelevu.

WHO yatoa muongozo wa kusaidia uangalizi wa afya ya akili kwa kina mama waliojifungua

Takriban mwanamke mmoja kati ya watano atapata tatizo la afya ya akili wakati wa ujauzito au mwaka mmoja baada ya kujifungua,  limesema leo shirika la Umoja wa Mataifa la afya Ulimwenguni WHO.

Bila uwekezaji, usawa wa kijinsia utachukua karibu miaka 300: Ripoti ya UN

Kwa maendeleo ya sasa, ripoti ya Umoja wa Mataifa inabainisha kuwa  lengo la 5 la maendeleo endelevu, SDG 5 ya Ajenda 2030 haliwezi kufikiwa; mapengo katika ulinzi wa kisheria na kuondolewa kwa sheria za kibaguzi yanaweza kuchukua hadi miaka 286 kuzibwa; majanga mengi na hasara katika haki za afya ya ngono na uzazi vinafuta maendeleo. 

UNICEF yawasilisha sehena ya misaada kwa ajili ya watoto na wanawake walioathirika na mafuriko nchini Pakistan

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto duniani UNICEF hii leo limewasilisha tani 32 za dawa za kuokoa maisha na vifaa vingine vya dharura ili kusaidia watoto na wanawake walioathiriwa na mafuriko kote nchini Pakistan.

UNFPA yaomba msaada wa dola mil 10.7 kusaidia wanawake na wasichana wa Sri Lanka

Shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu na afya ya uzazi UNFPA, limetoa ombi la dola milioni 10.7 kwa ajili ya kutoa usaidizi wa kuokoa maisha kwa wanawake na wasichana zaidi ya milioni mbili nchini Sri Lanka. 

Shule ya Kakenya Dream yazidisha mapambano dhidi ya mila potofu kwa jamii za kimasai

Kenya ni moja ya nchi za kwanza barani Afrika kuridhia mkataba wa kulinda haki za watoto wa Umoja wa mataifa. Ijapokuwa hatua zimepigwa kuimarisha hali ya watoto bado kazi ipo zaidi inayohitaji kufanywa na jamii kwa ujula ili kulinda maslahi ya watoto.

UNFPA yatangaza washindi 10 wa miradi ya kuwawezesha wanawake na wasichana

Shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu na afya ya uzazi UNFPA, leo limetaja washindi 10 wa pamoja wa shindano la miradi bunifu inayoweza kuleta mabadiliko chanya na kuwezesha wanawake na wasichana duniani. 

Kesi za unyanyasaji kingono zaongezeka kwa asilimia 218 nchini Sudan Kusini

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Sudan Kusini UNMISS umeeleza kuwa na wasiwasi mkubwa kutokan na kuongezeka kwa kesi za unyanyasaji wa kingono unaohusiana na migogoro zinazoibuka licha ya kupungua kwa jumla kwa idadi ya raia walioathiriwa na ghasia nchini humo.

Takriban nusu ya watoto wenye UKIMWI hawapati matibabu

Wakati zaidi ya robo tatu ya watu wazima wote wanaoishi na Virusi vya UKIMWI VVU wanapata aina fulani ya matibabu, idadi ya watoto wanaofanya hivyo, inafikia asilimia 52 pekee.