Katika nchi zinazoendelea, vifo vya wanawake vitokanavyo na kutokwa na damu nyingi baada ya kujifungua linaendelea kuwa mwiba kutokana na changamoto ya uhifadhi wa dawa ya kuzuia tatizo hilo.
Wataalamu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa wamesema hatua za haraka zinahitajika ili kuondokana na tabia inayotishia mafanikio ya haki za wanawake duniani yaliyopatikana kwa jasho.
Ukatili wa kingono katika migogoro ya vita ni tatizo lililomea mizizi na sio kwa wanawake peke yao, wanaume na watoto wametumbukizwa pia katika zahma hiyo kama anavyofafanua wakili Ann N. Kamunya raia wa Kenya ambaye sasa huyo Ankara Uturuki akifanya kazi na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR