Mradi wa huduma ya simu namba 116 inayotumiwa bure kutoa taarifa taarifa za matukio ya unyanyasaji kwa mtoto, mradi unaofadhiliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu UNFPA Tanzania unaendelea kuwa msaada wa kupambana na ukatili dhidi ya watoto nchini Tanzania.
Janga la ugonjwa wa virusi vya Corona, au COVID-19 limefichua siyo tu hatari zinazowakumba wazee bali pia mchango wao adhimu katika kulea wajukuu zao. Hivyo ndivyo kwa Ruth Sandrum kutoka Malawi ambaye yeye anajivunia kuwa mlezi wa wajukuu zake.
Harakati za Umoja wa Mataifa za kutekeleza lengo namba 5 la malengo ya maendeleo endelevu, SDGs la usawa wa jinsia na uwezeshaji wanawake linaendelea kupigiwa chepuo na wadau mbalimbali likiwemo shirika la kiraia la Naserian wilayan Monduli mkoani Arusha nchini Tanzania.
Mradi wa FISH4ACP ambao una lengo la kuimarisha uvuvi na ufugaji samaki barani Afrika, Karibea na Pasifiki ukifadhiliwa na shirika la chakula na kilimo la Umoja wa Mataifa FAO, umesaidia kuinua uchumi kama anavyoeleza mmoja wa wanufaika nchini Nigeria Bi Yahya Olunbumi.
Ujuzi uliopatikana kutokana na mafunzo yaliyotolewa kupitia mpango wa msaada wa kifedha kutoka mfuko wa Umoja wa Mataifa wa maendeleo ya chakula na kilimo, IFAD, umewawezesha wanawake katika jimbo la Niger nchini Nigeria kuvuka katika kipindi kigumu cha COVID-19 huku biasahara yao ya mchele ikizidi kushamiri.
Wanawake wakimbizi wa ndani kwenye eneo la Malakal nchini Sudan Kusini wanasema wamechoshwa na vita na kupoteza watoto wao kila uchao, sasa wanaitaka serikali kupanda mbegu ya amani na kusikiliza vilio vyao japo mara moja.
Kutana na Fiona Beine mmoja wa wanawake wanaotoa mchango mkubwa katika operesheni za ulinzi wa amani za Umoja wa Mataifa. Hivi sasa yeye ni naibu mshauri wa masuala ya usalama kwenye kwenye idara ya usalama ya mpango wa Umoja wa Mataifa nchini Iraq UNAMI.
Hii leo mkutano wa 75 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, UNGA75 unakuwa na kikao cha ngazi ya juu kuhusu kuchagiza utekelezaji wa usawa wa jinsia na uwezeshaji wanawake na mtoto wa kike, sambamba na maadhimisho ya miaka 25 tangu mkutano wa 4 wa kimataifa kuhusu wanawake uliofanyika Beijing nchini China mwaka 1995.
Mwanamuziki Yemi Alade, raia wa Nigeria ambaye hivi karibuni ametangazwa kuwa Balozi mwema wa shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa maendeleo UNDP amesema malengo ya UNDP yanaendana na malengo yake kwa hivyo atajitolea kwa uwezo wake wote.
Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF, limepeleka misaada katika eneo la Jebel Marra, Darfur, Sudan ili kuokoa maisha ya watu waliokimbilia katika maeneo hayo ya milima kuyakimbia mapigano katika maeneo yao.