Nchini Tanzania, taasisi ya kijamii ya Tanzania Youth Aviation, yenye lengo la kuhamasisha vijana na watoto kuingia katika faniya urubani na uongozaji wa ndege imeanza kufanikiwa katika kufikia lengo lake hilo wakati huu ambapo Umoja wa Mataifa na wadau wanataka wasichana nao wajiunge na masomo ya sayansi, teknolojia na hisabati, STEM.