Takwimu za Umoja wa Mataifa zinaonesha kwamba asilimia 78 ya wanawake walio ndani ya ndoa au wanaoishi katika mazingira ya ndoa wanaweza kupata huduma za mpango wa uzazi, hii ikiwa ni ongezeko la asilimia 72 tangu mwaka 1994, lakini idadi hiyo inapungua hadi chini ya asilimia 50 katika mataifa 44, mengi yakiwa Afrika kusini mwa jangwa la Sahara na mataifa ya kusini mwa visiwa vya pacific.