Ainisho la suala la usawa wa kijinsia limekuwa likileta utata hasa pale ambapo jamii haijaweza kushirikishwa vyema kutambua manufaa ya suala hilo. Huko wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma nchini Tanzania, suala hilo ambalo ni lengo namba tano la malengo ya maendeleo endelevu, SDGs sasa limeanza kushika kasi.