Umoja wa Mataifa unahimiza kuleta maendeleo kupitia malengo yake ya maendeleo endelevu SDGs.Mathalani lengo namba moja la kutokomeza umaskini kwa ifikapo mwaka wa 2030. Kwa mantiki hiyo wanawake wa wilaya ya Lwengo, Kusini mwa Uganda nao wameamua kujifunga kibwebwe kuweza kutokomeza umaskini . Wameanzisha soko lao ambalo linauza bidhaa mbalimbali za matunda kama vile nyanya , na mboga za majani. Siraj Kalyango amevinjari eneo hilo na kuzungumza na baadhi ya wanawake hao na kutuandalia Makala ifuatayo.