Mkutano wa kamisheni ya hali ya wanawake duniani kikao cha 65 umefungua pazia hii leo ikiwa ni mara ya pili kufanyika katika mazingira ya janga la virusi vya corona au covid-19 ambapo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema janga hili lina sura ya mwanamke akisema kwamba hali ya sasa imedhihirisha jinsi ukosefu wa usawa wa kijinsi ulivyo kwa kiasi kikubwa na umekita mizizi katika mifumo ya kisiasa, kijamii na kiuchumi.